Mwimbaji Staa wa Bongofleva Rayvanny anae-trend na goma jipya la 'number one' remix ft. Enisa, amemuomba radhi Mwigizaji Kajala kufuatia video zilizosambaa zikiwaonesha Rayvanny na Mtoto wa Kajala aitwae Paula mwezi uliopita.
Rayvanny ameandika ———> “Duniani wakati mwingine kuna vitu tunavifanya ambavyo pengine kwa macho yetu ya ujana tunaona ni sahihi lakini tunasahau upande mwingine wa pili ambao ni wazazi wanaoumia kwa namna moja au nyingine”
“Nichukue nafasi hii kumuomba radhi dada angu Kajala na kuwaomba radhi Wazazi na yoyote ambaye nilimkwaza kwa kupost video ambayo inawezekana imetafsiriwa vibaya ...kwasababu sisi ni binadamu na kamwe hatuwezi kukamilika” ——— Rayvanny.
