Haipingiki Smart phones zimerahisisha sana maisha na kutuwezesha kufanya vingi ambavyo hatukuweza kuvifanya kwa simu zamani, tunafurahia kupiga picha, kupigiana hadi video, kutumia internet na mengine mengi ya faida lakini kuna hasara kubwa tunaweza kuipata kwa kutumia smartphone hizi kama hatutozingatia anachokisema huyu Daktari na kuelekeza kwa njia ya video.
Dr. Cyprian Mtomoka anasema "Macho huwa yana uteute flani ambao kazi yake ni kuyalainisha, sasa ukikaa kwenye kifaa chenye mwanga mkali kama hivyo ule mwanga mkali unakausha ule uteute na ukishapungua Mtu anapata madhara ya kushindwa kuona"
“Wengine wanatazama movie wakiwa wamezima taa, unapoangalia ukiwa gizani ule mwanga unakua mkali zaidi kuliko ukiwa kwenye taa, ufumbuzi ni kufanya yafuatayo mfano ukitumia computer kwa dakika 20 hakikisha unahamisha macho yako futi 20 kwenda sehemu nyingine ili uweze kupiga kope mara 20”
“Hiyo inasaidia kurejesha jicho kufanya kazi vizuri, tunashauri pia mtumie settings za kupunguza mwanga kwenye vifaa hivyo" #MillardAyoKURUNZI
DW Kiswahili

