Ampiga ngumi ya uso mamba aliyekuwa akimshambulia dada yake

0
Melissa na Georgia Laurie

CHANZO CHA PICHA,HANA LAURIE

Wakati mamba alipomkamata dada yake, kulikuwa na chaguo moja tu kwa Georgia Laurie - alimpiga ngumi ya uso.

Mapacha hao wa miaka 28 walikuwa wakiogelea Mexico wakati Melissa alipoburuzwa chini ya maji na mnyama huyo.

Ndugu hao, kutoka Berkshire, walikuwa katika ziwani karibu na mji wa Puerto Escondido, Jumapili, wakati shambulio hilo lilipotokea.

Walikuwa wakisafiri, wakijitolea na kufanya kazi katika hifadhi za wanyama - dada yao Hana anaiambia Radio 1 Newsbeat.

'Alianza kumpiga'

Dada wote wawili, ambao wanaishi Berkshire, sasa wako hospitalini huko Mexico - na Melissa kwa sasa wamempa dawa ya usingizi, kwa sababu ya wasiwasi kutokana na majeraha aliyopata.

Wakati walipokuwa wanaogelea, Melissa alitoweka chini ya maji na Georgia alikuwa akijaribu kumtafuta.

Mamba hujaribu kuwazamisha waathiriwa.

"Georgia alimkuta hana fahamu na akamburuza mpaka kwenye mashua," anasema Hana mwenye miaka 33 akiwa nyumbani kwake Alton, Hampshire.

"Alivuta akiwa amemshika mgongoni kwani mamba aliendelea kumfuata- kwa hivyo alianza kumpiga.

"Alikuwa amesikia kuwa kwa wanyama wengine, ndivyo unavyolazimika kufanya."

Hana anasema Melissa alitupwa na mamba kama ''mwanasesere''.

Melissa na Georgia Laurie

CHANZO CHA PICHA,HANA LAURIE

Madaktari wana wasiwasi juu ya maji ambayo akina dada walikuwa wakiogelea, na vile vile chochote ambacho kingeweza kupitishwa kutoka kwenye mdomo na meno ya mamba.

Melissa ana maji kwenye mapafu yake na labda mapafu yaliumwa pia. Hivi sasa anapokea msaada wa kupumua.


"Wote Georgia na Melissa wako kwenye dozi nzito za dawa, kwa hivyo tunatumaini kuwa ikiwa maambukizi yoyote yatajitokeza wataweza kugundua haraka sana," anasema Hana.

'Alipata ujasiri'

Hana anasema Georgia ni mpigambizi mwenye uzoefu, lakini ''aliingiwa hofu'' alipokabiliana uso kwa uso na mamba.

''La kushukuru ni kuwa alikuwa na mafuzo. ghafla alipata ujasiri na alijua cha kufanya.''

Familia ya Laurie

CHANZO CHA PICHA,HANA LAURIE

Lakini wameweza kuzungumza na Georgia kwa WhatsApp na amepiga simu za video kutoka kitandani hospitalini.

"Georgia anapata taarifa za maendeleo yake mara kwa mara kutoka kwa madaktari wanapokuja kumuona, juu ya hali ya Melissa. Ni ngumu," anasema Hana.

"Yeye ni jasiri sana na nadhani bado ana mshtuko. Lakini ilibidi nimwambie tu jinsi nilivyojivunia yeye.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable