Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu Mmiliki wa Kampuni ya Kufua umeme ya IPTL, Harbinder Seth kulipa fidia ya Shilingi BILIONI 26 za Kitanzania baada ya kupatikana na hatia ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi leo ambapo amesema ——— > “Ni dhahiri umekaa mahabusu kwa muda mrefu takribani miaka minne ni muda mwingi wa kutosha na ni wazi umeona mengi na kujifunza mengi ukiwa gerezani”
"Pia kwa mantiki hiyo Mahakama inaamua kukupa onyo usije ukatenda makosa tena na utakuwa chini ya uangalizi kwa muda wa mwaka mmoja hayo ndio maamuzi ya Mahakama, kuhusu nyaraka mbalimbali ikiwemo Passport ya kusafiria arudishiwe” - Hakimu Huruma Shaidi.
