Eriksen alihitaji huduma ya dharura uwanjani kabla ya kupelekwa hospitalini
Christian Eriksen anaendelea kupata ahueni hospitalini na ametuma salamu zake kwa wachezaji wenzake wa timu ya mpira wa miguu ya Denmark.
Eriksen alianguka muda mfupi kabla ya mapumziko katika mchezo wa ufunguzi wa michuano ya Euro 2020 ambapo Denmark ilikuwa ikichuana dhidi ya Finland Jumamosi usiku.
Mchezaji huyo wa Inter Milan mwenye umri wa miaka 29 alipata matibabu ya dharura uwanjani kabla ya kupelekwa hospitalini alikolazwa.
"Hali yake ni sawa na anaendelea kulazwa hospitalini kwa uchunguzi zaidi," ilisema taarifa ya shirikisho la mpira wa miguu la Denmark.
"Leo asubuhi tumezungumza na Christian, ambaye ametuma salamu zake kwa wachezaji wenzake.
"Timu na wafanyikazi wa timu ya kitaifa wamepokea ushauri nasaha baada ya kushuhudia tukio hilo uwanjani na wataendelea kupeana motisha baada ya tukio la jana.
"Tungependa kumshukuru kila mtu kwa salamu zao za dhati."
Tukio la Jumamosi lilitokea wakati mpira ulipigwa kuelekea kwa Eriksen karibu na mwisho wa kipindi cha kwanza.
Wenzake waliofadhaika walimzunguka kumpa faragha japo katika hali ile mashabiki katika uwanja wa Parken walionekana kukasirika wakati mchezaji huyo alipotibiwa.