Mara moja moja, mshauri wake humuonesha video ya mtandaoni ya kumdhihaki yeye na serikali yake.

Rais wa Urusi ni mtu wa kufanya kazi sana usiku na mara nyingi huchelewa sana kulala akifanya kazi. Hufanya kazi zake vyema usiku, uliandika mtandao wa habari wa Urusi wa Newsweek.

Inakuaje anaposafiri nje ya nchi?

Wakati anaposafiri nje ya nchi, ratiba ya Rais Putin ya siku huwa imesheheni mambo mengi zaidi. Kokote anakopokelewa kila kitu hubadilishwa kuanzia shuka, sabuni, vifaa vya usafi hadi mabakuli ya matunda.

Putin pia huwa hakubali chakula kilichoandaliwa na mwenyeji wake ambacho hakijaidhinishwa na Kremlin.

Putin hupenda mvinyo baada ya chakula

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Putin hupenda mvinyo baada ya chakula

Awali jarida la The Telegraph liliripoti kuwa chakula anachokipenda zaidi Bw Putin ni Ice Cream aina ya pistachio . Aliwahi pia kumpatia zawadi rais wa uchina Xi Jinping aina hiyo ya ice cream wakati wa mkutano wa G20 summit wa mwaka 2017.

Miaka kadhaa iliyopita mgahawa wa St. Petersburg Podvorye ulikuwa na menyu iliyoitwa -Mlo wa mchana wa Vladimir Putin "The Lunch of Vladimir Putin" - ambao ulitengeneza chakula alichokipenda raisi huyo wa Urusi. Mara nyingi alikuwa akiagiza pale nyama inayoitwa "frying pan," yenye mchanganyiko wa vipande vya nyama vilivyokatwa katwa kwa umbo la ulimi, soseji, vipande vyembamba vya nyama isiyo na mifupa, na mikate ya kuokwa iliyochanganywa na mboga.

Mwaka 2010, mpishi wa Kremlin Anatoly Galkin alisema kuwa Bw Putin anapendelea mvinyo au bia.

Baadhi ya vyombo vya habari vinadai kuwa rais huyo huburudishwa kwa mvinyo mwekundu wa Uhispania- Spanish red wines, huku baadhi vikidai hupenda kunywa kiasi kidogo cha Vodka baada ya chakula.

Ratiba ya kazi yake siku za wikendi huwa haina mambo mengi ya kufanya, ili kumpatia muda Bw Putin kuhudhuria mafunzo yake ya lugha ya Kiingereza. Jumapili wakati mwingine husali na kuungama.

Hatahivyo, maafisa wa Urusi ambao wako karibu na rais huyo wanasisitiza kuwa yeye sio Mkristo ," kulingana na gazeti la Newsweek.

Kila baada ya wiki chache, ratiba ya Bw Putin husititishwa ili kutoa fursa ya muda wake wa kibinafsi wa kucheza hockey, mchezo wa kuteleza kwenye barafu.

Putin akiwa na mbwa wake Buffy na Yume

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Putin akiwa na mbwa wake Buffy na Yume

Rais huyo wa urusi hatazami tu mchezo, bali anacheza katika ligi, huku akizungunga dhidi ya miraba ya timu za walinzi wake.

Putin pia anawapenda wanyama. Anamiliki mbwa mweusi aina ya Labrador anayeitwa Konni, Yume wa aina ya Akita Inu , na mbwa aina ya Karakachan anayeitwa Buffy.