Gosiame Thamara Sithole katika pich iliopigwa mwezi mmoja uliopita, alijifungua siku ya jumatatu.
Mwanamke wa Afrika Kusini ameripotiwa kujifungua watoto, idadi hiyo ikiwa inaweka rekodi mpya duniani.
Mume wake Gosiame Thamara Sithole anasema walishangazwa na idadi hiyo ya watoto baada ya picha ya scan kuonesha kuwa alikuwa na watoto wanane tu tumboni mwake.
"Ni wavulana saba na wasichana watatu. Ninafuraha. Ninahisia. Siwezi kuzungumza mengi,'' mumewe Teboho Tsotetsi aliiambia Pretoria News. Baada ya kuzaliwa kwa watoto hao.
Afisa mmoja wa Afrika Kusini aliithibitishia BBC kuhusu kuzaliwa kwa watoto hao, hatahivyo mwingine alisema bado hawajawaona watoto hao.
Mmoja wa watu wa familia yao, ambaye hakutaka kutambuliwa, aliiambia BBC kuwa Bi Sithole alipata watoto 10- watano alijifungua kwa njia ya kawaida na watano wengine kwa njia ya upasuaji
Taasisi ya Rekodi ya dunia ya Guinness iliiambia BBC kuwa inachunguza kisa cha Bi Sithole.
Kwa sasa mwanamke wa Marekani ambaye alijifungua watoto wanane ndiye anayeshikilia rekodi ya Guiness ya mtu aliuyejifungua watoto wengi zaidi mara moja anayeishi.
Mwezi uliopita, mwanamke mwenye umri wa miaka 25 halima Cisse kutoka nchini Mali alijifungua watoto tisa, ambao wanaripotiwa kuendelea vyema katika kliniki nchini Morocco.
Mimba nyingi za idadi kubwa ya watoto huishia kujharibika, anasema mwandishi wa BBC wa masuala ya afya, Rhoda Odhiambo.Most pregnancies involving large numbers of babies end prematurely, says BBC Africa's health reporter Rhoda Odhiambo.
Uzazi wa watoto zaidi ya watatu ni nadra na mara nyingi hutokana na matibabu ya uzazi-lakini katikakisa hiki wanandoa hao wanasema walipata ujauzito kwa njia ya kawaida .
Maombi na kukosa usingizi usiku
Bi Sithole mwenye umri wa miaka 37, awali alijifungua watoto mapacha ambao kwa sasa wana umri wa miaka sita.
Alisemekana alikuwa mzima mwenye afya baada ya kujifungua wiki 29 baada ya ujauzito wa wiki 29 mjini Pretoria .
Akizungumza na Pretoria News mwezi uliopita, Bi Sitholealisema ujauzito wake ulikuwa "mgumu mwanzoni'' na alikuwa akisali ajifungue watoto wenye afya, huku akishindwa kulala usiku mara nyingijuu ya kile kitakachotokea.
"Ni vipi watatoshea tumboni mwangu? Wataweza kuishi vipi?" alijiuliza mwenyewe, lakini alihakikishiwa na madaktari kwamba kizazi chake kilikuwa kinapanuka.
Picha
Wakati huo ilifikiriwa kuwa alikuwa na mimba ya watoto wanane, Bi Sithole alikuwa anaumwa miguu na madaktari walibaini watot wawili kati ya wanane ''walikuwa katika mrija usio sahihi ".
"Hilo lilitatuliwa na nimekuwa sawa tangu wakati huo. Natamani kuwaona watoto wangu," aliliambia gazeti wakati huo.
Mume wake pia alisema alikuwa mwenye furaha ya kupindukia, na nilihisi kama "mmoja wa watoto waliochaguliwa na Mungu. Ni muujiza ambao ninaushukuru ".
Maombi na kukosa usingizi usiku
Bi Sithole mwenye umri wa miaka 37, awali alijifungua watoto mapacha ambao kwa sasa wana umri wa miaka sita.
Alisemekana alikuwa mzima mwenye afya baada ya kujifungua wiki 29 baada ya ujauzito wa wiki 29 mjini Pretoria .
Akizungumza na Pretoria News mwezi uliopita, Bi Sithole alisema ujauzito wake ulikuwa "mgumu mwanzoni'' na alikuwa akisali ajifungue watoto wenye afya, huku akishindwa kulala usiku mara nyingi juu ya kile kitakachotokea.
"Ni vipi watatoshea tumboni mwangu? Wataweza kuishi vipi?" alijiuliza mwenyewe, lakini alihakikishiwa na madaktari kwamba kizazi chake kilikuwa kinapanuka.
Mimba nyingi zinazohusisha watoto wengi huishia bila mafanikio ya kupata watoto
Wakati huo ilifikiriwa kuwa alikuwa na mimba ya watoto wanane, Bi Sithole alikuwa anaumwa miguu na madaktari walibaini watoto wawili kati ya wanane ''walikuwa katika mrija usio sahihi ".