Hija 2021: Ni Wakazi wa Saudi Arabia watakaofanya Hija ya mwaka huu

0
Maafisa nchini Saudi Arabia wamesema ni watu 60,000 tu watakaoruhusiwa kufanya hija

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Maafisa nchini Saudi Arabia wamesema ni watu 60,000 tu watakaoruhusiwa kufanya Hija

Maafisa nchini Saudi Arabia wamesema ni watu 60,000 tu watakaoruhusiwa kufanya Hija, kulingana na wavuti wa Haramain Sharifain, ambao unaripoti kutoka katika misikiti miwili mitakatifu.

Aidha taarifa hiyo inasema ni wakazi wa Saudi Arabia pekee watakaoruhusiwa kufanya Hija mwaka huu, wakiwemo wa wageni wanaoishi nchini humo.

Wavuti huo unasema kuwa hatua hiyo imechukuliwa kutokana na kusambaa kwa aina mpya za virusi ya corona kote duniani.

Mwaka jana Saudi Arabia pia ilipiga maarufuku raia kutoka mataifa mengine kufanya ibada ya Hija nchini humo ili kudhibiti virusi vya corona.

Mahujaji wakiwa msikiti wa Makka, Saudi Arabia

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Watu takriban milioni mbili, huenda Maka na Madina kwa ajili ya kufanya hija

Watu takriban milioni mbili vinginevyo wangetembelea Maka na Madina msimu wa kiangazi kwa ajili ya Hija hiyo inayofanyika kila mwaka kulingana na imani ya kiislamu.

Kumekuwa na hofu kwamba Hija inaweza kufutwa kabisa.

Kwa kawaida Hija ni moja ya vipindi muhimu katika kalenda ya dini ya Kiislamu. Lakini ni raia kutoka nchi nyingine ambao tayari ni wakazi wa Saudi Arabia watakaoruhusiwa kuhudhuria Hija ya mwaka huu.

Waumini wakisali kwa kuzingatia amri ya kutokaribiana mjini Mecca mwezi Aprili

CHANZO CHA PICHA,AFP

Maelezo ya picha,

Waumini wakisali kwa kuzingatia amri ya kutokaribiana mjini Mecca mwezi Aprili

Maafisa nchini humo wanasema hii ndio njia pekee itakayowezesha kufanya mipango ya kutokaribiana ambayo itawezesha watu wawe salama.

Saudi Arabia imerekodi visa vya corona 161,005 na vifo vilivyotokana na ugonjwa huo ni 1,307.

Iliweza kuondoa amri ya kutotoka nje mwishoni mwa juma.

Hijj ni nini?

Hija ni mojawapo ya nguzo tano za Kiislamu ambayo kila Muislamu hutakiwa kuitekeleza walau mara moja.

ramani

Kila Muislamu, mwenye afya nzuri na aliye na uwezo anapaswa kutimiza nguzo hii ili kuishi maisha mazuri na ya uwajibikaji, kwa mujibu wa dini ya Kiislamu.

Mahujaji hukusanyika mjini Mecca kusimama mbele ya Kaaba, wakimsifu Allah (Mola) Mungu pamoja.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable