Hatua ya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kuwakataa majaji sita waliopendekezwa na Tume ya Hudama za Mahakama,JSC, imeendelea kuzua hisia mseto.
Kiongozi wa hivi punde kutoa kauli yake kuhusiana na suala hilo ni Jaji Mkuu mshaafu David Maraga.
Katika mahojiano na Kituo cha Televisheni cha KTN, Bwana Maraga alisema: ''Hali kama hii ikiendelea nchini itaongozwa bila katiba''
Maraga amemtaka rais Kenyatta kuwateua majaji sita aliowaacha nje.
''Muda umewadia kwa bunge kumuondoa madarakani (Uhuru) akikiuka katiba'' aliongeza kusema.
Majaji hao sita ni miongoni mwa majaji 41 ambao walikuwa wamependekezwa kwa ajili ya uteuzi na Tume ya Huduma za mahakama nchini humo (JSC) miaka miwili iliyopita. Mmoja wa majaji hao alifariki.
Rais Kenyatta amekataa mapendekezo ya JSC licha ya maagizo mawili ya mahakama yaliyomtaka kufanya hivyo.
