Karina Nunez na mwanawe Valesco
Karina Núñez ni kizazi cha nne cha familia ya makahaba kutoka Uruguay na anakumbuka maisha yake ya utotoni yalivyokuwa na panda shuka za kila aina.
"Zama za utawala wa kidikteta wa kijeshi nchini Uruguay, mwanamume mmoja alimchukua mama yangu kutoka kwa gawadi wake na kuamua kunilea mimi kama binti yake," alisema katika mahojiano na BBC Mundo.
"Baadaye alipokuwa mfungwa wa kisiasa maisha yetu yalibadilika kabisa: mama yangu alirejelea maisha ya ukahaba."
Ijapokuwa maisha yake ya utotoni hayakuwa rahisi, anayaelezea kuwa mchanganyiko wa umasikini, kutokuwa na matumaini na isipokuwa kufanya ukahaba, Leo anasema "amekata minyororo hiyo."
Ndio ukweli wa mambo. Amekuwa mmoja wa viongozi mashuhuri wa muungano wa wafanya kazi nchini Uruguay.
Kando na kutetea haki ya wanawake wanaofanya biashara ya ngono, Karina pia anakabiliana na unyanyasaji wa kingonoo dhidi ya watoto na watu wazima.
Pia, "kwa kushirikiana na wanawake," amefanikiwa kumwezesha binti yake, Valeska, kuwa mtu wa kwanza katika familia yake kujiunga na taasisi ya elimu, hatua ambayo anajivunia sana. Lakini safari hiyo haikuwa rahisi
"Ukizaliwa katika mazingira ya ukahaba, ni vigumu sana kuondoka katika mazingira hayo."
Kila wakati nilifikiria usipojitetea ukipatikana na tatizo lolote, basi utajilaumu mwenyewe kwasababu ni maisha uliyojichagulia na huna budi kuyaishi.
Ulifanya uamuzi mbaya na huna budi kuvumilia
Sikuchukulia kwamba mambo yaliyonikuta maishani ni matokeo ya kuwa katika mazingira ya ukahaba kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
Hali ya kudhulumiwa kingono niliyoishi nayo kwa muda mrefu ilinifanya nifikirie ni ushujaa.
Miaka kadhaa baadaye nimefahamu kwa machungu kwamba kutumika kingono sio jambo la kujivunia kushujaa.
Uelewa huo umenisaidia kusalia katika nafasi ya muathirika na kujiimarisha mimi binafsi ili baadaye niweze kuwawaokoa wenzangu wanaopitia hali hiyo ngumu kimya kimya.
Kila mtu ana namna yake ya kuamua mazingira anayoishi ni salama kiasi gani.
Kwa wengine wetu tuliyolelewa katika mazingira ya kutoa huduma za ngono na mahali ambapo kuzungumzia huduma za ngono ni jambo la kawaida, bila shaka hatuwezi kutafuta mahali pengine pa kuishi.
"Nilitaka kuwa kielelezo chema cha Valesca"
Karina Nuñez hakutaka binti yake kufuata mkondo wake wa maisha, au hata wa bibi yake, baada ya kuishi maisha ya ukahaba na kushuhudia changamoto wanazopitia kila siku.
Kila nilipobisha milango kutetea haki ya wafanyakazi wenzangu , walinitambua kama mtetezi wao wa kuaminika.
Walinipatia jina la mtetezi na majina mengine mengi, lakini ukweli ni kwamba nilitaka kuleta mabadiliko kwa kuwa mfano mzuri zaidi wa Karina.
Mwaka 1999, Nilipinga mtandao wa walanguzi wa watu uliowapeleka (wasichana) Italia na kutokana na hilo nilipewa kichapo kibaya na maafisa tisa wa mtandao huo. Nililazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi kwa siku 11 na ilinichukua miezi mitatu kuweza kutembea tena.
Nilipofanikiwa kutembea kwanza kutumia magongo, nilirejelea tena harakati zangu na kumshtaki mlinzi aliyeniuza kwa mtandao huo.
Leo najivunia juhudi hizo zilifua dafu.
"Tofauti ya maadili kati ya mwanamke mtakatifu na kahaba"
Nchi Uruguay, ukahaba ni shughuli ambayo imehalalishwa tangu 2002 na ni moja ya mataifa ya America Kusini ambayo yana sheria huria kuhusiana na suala hilo.
Katika baadhi ya nchi katika eneo hilo bado zina mianya ya kisheria inayowapatia watu nafasi ya kufanya ukahaba lakini katika nchi zingine ukahaba umeharamishwa.
Karina anafikikiria kuwa hii inatokana na mitazamo ya kimaadili "ambayo tumekuwa nayo, kutoka kwa Bibilia na na kutoka Agano Jipya."
"Kuna tofauti kati ya mwanamke mtakatifu na kahaba."
Karina Nunez ni mpiganajji wa haki za wanawake
Ijapokuwa sasa anajichukulia ''kuwa na mtazamo tofauti' anakiri kuwa ilimchukua muda mrefu kulitambua hilo
"Bado anapata changamoto kutambuliwa kama mtetezi wa wanawake. Nadhani Amerika Kusini bado kuna haja ya kuwa na mjadala wa wazi kuhusu suala la ukahaba na uhuru wa kujiamulia wanachokitaka kufanya na miili yao."
Hatua tatu ya ukahaba
Kulingana na Karina Núñez, makahaba wengi wanapitia hatua tatu ya kazi hiyo. Hitimisho ambalo lilifikiwa baada ya kuwahoji wafanyakazi wa ngono karibu elfu mbili.
Wote walijaza fomu lakini utafiti wake uliwaangazia wanawake 313 ambao walifanya ukahaba mpaka wakafika mwisho wake.
Karina anasema kwamba Makahaba ni wanawake walio na ujasiri
Matokeo ya utafiti huo ulichapishwa katika kitabu "kinachoangazia masuala ya ukahaba", ambacho kwa sasa kiko katika toleo la tatu.
Kulingana na mimi… Nilipoandika kitabu hicho mwaka 2008, ukahaba kwangu ulikuwa kutoa huduma za kingono.
Baadaye nikajua ukifanya ukahaba kabla hujatimiza miaka 18 ilikuwa ni unyanyasaji wa kingono na wala sio aina ya kazi.
Ni ukiukaji wa haki za watoto.
2. Katika hatua ya pili ya ukahaba. Hata mwanamke anajielewa, kiasi cha kuwa anajua umuhimu wa huduma anayotoa, kwasababu mbeleni alikubali kutumika vibaya na kuingiliwa bila kujali.
Lakini katika hatua hii, yanaweza kumlipisha mteja kabla ya kukubali kufanyiwa mambo mengine na pia anaweza kudhibiti kiwango cha huduma anayotoa.
Nchini Uruguay ambako ukahaba unadhibitiwa, wanaofanya kazi hiyo wanatakiwa kupata leseni baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.
Lakini, uchunguzi umebaini kuwa wale ambao hawajamaliza masomo ya msingi au ya upili walifanya ukahaba maisha yao yote.
Walitoa huduma ya kingono bila kuzingatia huduma za kimatibabu
Wale ambao wamesoma hadi kiwango cha chuo kikuu, walifanya kazi hiyo kwa kati ya miaka 10 hadi 15.
Wale ambao hawana kisomo waliishia kuwa makahaba hadi wakazaa watoto wa kike ambao pia wamejipata wakifanya kazi kama ya mama zao au watoto wa kiume ambao wanafanya shughuli za kuwatafutia soko makahaba na biashara zingine haramu.
Na wale ambao walikuwa na kiwango cha juu cha masomo watoto was hawajipati katika hali hizo siku za usoni.


