Kenya: Rufaa ya BBI yaanza kusikilizwa

0
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta (Kushoto) anyoosha mkono wa salamu kwa kiongozi wa upinzani Raila Odinga (Kulia) mjini Nairobi, Machi 9, 2018.

Mahakama ya rufaa ya Kenya, Jumanne iliianza kusikiliza kesi inayoelezwa na wachambuzi kuwa yenye umuhimu mkubwa kwa mstakabal wa kisiasa nchini humo, iliyowasilishwa dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu, ambao ulisimamisha msukumo wa marekebisho ya katiba kupitia mpango maarufu kama BBI.

Jopo la majaji saba lilianza kusikiliza kesi hiyo leo asubuhi, na itaendelea kwa siku tano na hatimaye litaamua iwapo nchi hiyo itaitisha kura ya maoni ya kuifanyia Katiba marekebisho.

Viongozi wanaounga mkono BBI, wakiwa ni pamoja na Rais Uhuru Kenyatta, na kiongozi wa upinzani, Raila Odinga, wanatumai kuwa mahakama hiyo ya rufaa itasitisha utekelezaji wa uamuzi huo wa mahakama kuu.

Washirika hao wawili wa mpango wa maridhiano maarufu kama 'Handshake,' wamekuwa wakipigia upatu mchakato huo, wakisisitiza kuwa ni njia ya kuunganisha nchi, na kuimarisha mstakabali wa amani nchini humo. Mahakama kuu, ilitoa maamuzi kwamba mchakato huo ulikiuka katiba.

Wawili hao wanawakilishwa na mawakili sita.Tume ya uchaguzi na mipaka, IEBC, pia imejumuishwa kwenye rufaa hiyo.

Jopo hilo la mahakama ya rufaa linaongozwa na jaji Daniel Musinga.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable