Kesi ya uhalifu wa kivita dhidi ya kamanda wa zamani wa waasi Liberia kuamuliwa

0

Kesi ya uhalifu wa kivita dhidi ya kamanda wa zamani wa waasi Liberia kuamuliwa

Alieu Kosiah alishtakiwa katika mahakama ya Uswizi
Image caption: Alieu Kosiah alishtakiwa katika mahakama ya Uswizi

Mahakama nchini Uswizi leo inatarajiwa kutoa uamuzi wa kesi inayomkabili kamanda wa zamani wa waasi huko Liberia.

Alieu Kosiah anatuhumiwa kwa kutekeleza makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu ikiwemo ubakaji na mauaji kati ya mwaka 1993 na 1996, wakati wa vita vya muda mrefu vya wenyewe kwa wenyewe. Amekana mashtaka hayo.

Bw. Kosiah aliyekimbilia nchini Uswizi kwa zaidi ya miaka 20 iliyopita alikamatwa mwaka 2014.

Ni raia wa kwanza wa Liberia kushtakiwa kwa uhalifu wa kivita unaohusiana na mzozo huo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable