Kwanini Kim Jong-Un anapiga vita lugha ya mitaani, nguo na filamu za nje ya nchi

0
Mr Kim has referred to foreign speech, hairstyles and clothes as "dangerous poisons"

CHANZO CHA PICHA,EPA

Hivi karibuni Korea Kaskazini imeanzisha sheria mpya nia ikiwa ni kukabiliana na ushawishi wowote ule kutoka nje ya nchi hiyo - adhabu kali itatolewa kwa yeyote atakayepatikana na filamu za nje ya nchi hiyo, mavazi au hata kutumia lugha ya mitaani. Lakini kwanini iwe hivyo?

Yoon Mi-so anasema alikuwa na miaka 11 aliposhuhudia kwa mara ya kwanza mwanamume akinyongwa kwa kosa la kupatikana na filamu ya Korea Kusini.

Kijiji chote kililazimishwa kutazama wakati adhabu inatolewa.

"Na kama haungeitazama, ilichukuliwa kama usaliti," aliiambia BBC akiwa nyumbani kwake mjini Seoul.

Though illegal, many in the North watch South Korean programmes

Vikosi wa Korea Kaskazini lilikuwa likihakikisha kila mmoja alijua kosa la kuingiza kimagendo video au filamu za nje ya nchi adhabu yake ni kifo.

"Nakumbuka vizuri kabisa mwanamume yule aliyekuwa amefungwa uso, lakini bado ningeweza kuona machozi yakimtiririka. Kumtazama, iliniumiza sana moyo. Kitambaa alichokuwa amefungwa kilikuwa kimelowa kabisa machozi.

"Walimfunga kwenye nguzo fulani na kumpiga risasi."

'Vita bila silaha'

Fikiria kuwa katika hali ya kufungiwa kila siku bila mtandao, hakuna kuingia kwenye mitandao ya kijamii na vituo vichache tu vya televisheni vilivyowekwa kutoa huduma hiyo wanasema yale ambayo viongozi wa nchi wanataka muyasikie - hayo ndio maisha ya Korea Kaskazini.

Na sasa hivi kiongozi wao Kim Jong-Un ameendeleza kubinywa zaidi na kuanzisha sheria mpya.

Yeyote atakayekamatwa na kiwango kikubwa cha data za vyombo vya habari kutoka Korea Kusini, Marekani na Japani sasa hivi atakabiliwa na adhabu ya kifo. Wale watakaokamatwa wanakabiliwa na kifungo cha miaka 15 gerezani.

Na sio tu kuhusu suala la kile ambacho watu wanatazama.

Hivi karibuni, Bwana Kim aliandika barua katika chombo cha habari kinachomilikiwa na serikali nchini humo, akitoa wito kuwa anataka kusitisha tabia "zisizofaa, ubinafsi na zisizopendelea ujamaa" miongoni mwa vijana. Anataka kusitisha maudhui kutoka nchi za kigeni, mitindo ya nywele na mavazi anayoelezea kama "sumu hatari".

Daily NK, tovuti moja mjini Seoul huku vyanzo Korea Kaskazini, ikiripoti kwamba vijana watatu walikuwa wametumwa tena katika kambi za kupata mafunzo tena kwa kosa la kunyoa nywele zao kama wanamuziki wa K-pop na kushona suruali zao juu ya magoti.

Lakini haya yote ni kwasababu Bwana Kim yuko vitani ambavyo havijumuishi silaha za nyuklia au makombora.

Wachambuzi wanasema anajaribu kusitisha taarifa kutoka nje kufikia watu wa Korea Kaskazini wakati maisha nchini humo yanaendelea kuwa magumu.

Inakisiwa kuwa mamilioni ya watu wanalala njaa. Bwana Kim anataka kuhakikisha kwamba wote wanapewa chakula ikiwa ni propaganda ya serikali.

Sheria hiyo inasema nini?

Gazeti la Daily NK la Korea Kaskazini lilikuwa la kwanza kupata nakala hiyo ya sheria.

"Inasema ikiwa mtu atapatikana, anaweza kuadhibiwa na ikiwa mtoto ndio tatizo, wazazi wanaweza kuadhibiwa. Mfumo wa kila mmoja kumfuatilia mwingine unaohamasishwa na Korea Kaskazini unaakisiwa katika sheria hii," Mhariri mkuu Lee Sang Yong amezungumza na BBC.

Anasema hatua hii inalenga "kuzima" ndoto zozote au matamanio wanayoweza kuwa nayo vijana kuhusu Korea Kusini.

Sometimes, TVs would be powered by car batteries

"Kwa maneno mengine, utawala uliopo ulisema kuwa unaweza kukumbana na upinzani ikiwa utamaduni wa nchi zingine utaruhusiwa kuingia nchini humo," alisema.

Choi Jong-hoon, mmoja kati ya wachache walioweza kutororoka nchini humo mwaka jana, ameiambia BBC kwamba "kadri wakati unavyoendelea kuwa mgumu, ndivyo kanuni, sheria na adhabu zinavyoendelea kuwa ngumu".

Je sheria hiyo itafanikiwa?

Kamata kamata zilizotangulia zilionesha vile watu walivyochangia katika kusambaza na kutazama filamu za kigeni ambazo kawaida huingizwa kimagendo kupitia mpaka wa China.

Kamata kamata ilianza lini?

Bwana Choi anakumbuka vikosi vya usalama vikivamia chuo kikuu karibu mwaka 2002 na kunasa zaidi ya kanda 20,000 za filamu.

"Hicho kilikuwa tu chuo kikuu kimoja. Sasa fikiria, zinaweza kuwa ngapi kote nchini humo? Serikali ilishtuka. Na hapo ndipo walihakikisha adhabu inakuwa kali zaidi," amesema.

Stairway to Heaven was a popular show in North Korea about 20 years ago

CHANZO CHA PICHA,SBS

Kim Geum-hyok anasema mwaka 2009 alikuwa na miaka 16 pekee alipokamatwa na maafisa wa kikosi maalum kilichokuwa kimeundwa kutafuta na kumkamata yeyote atakayepatikana akishirikisha wengine video zisizoruhusiwa nchini humo.

Alikuwa amempa rafiki yake DVD ya muziki aina ya pop ya Korea Kusini ambayo baba yake alikuwa ameiingiza kutoka China.

Alichukuliwa kama tu mkubwa na kupelekwa katika chumba cha pekee kuhojiwa. Anasema alipigwa mara kadhaa kwa siku nne.

"Niliogopa," ameliambia shirika la BBC kutoka Seoul anakoishi kwa sasa.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable