Rais wa Marekani Joe Biden leo anatarajiwa kukutana na Rais wa Urusi Vladmir Putin mjini Geneva Uswizi.
Viongozi hao wawili watakutana ana kwa ana kwa mara ya kwanza tangu Biden alipoinga madarakani na wadadisi wa wanasema huenda usiwe wa kirafiki.
Hii ni kwasababu,Urusi imejumuisha Marekani katika orodha yake rasmi ya ''mataifa yenye uhasama''
Uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili umezorota na kwa sasa hakuna balozi pande zote mbili; maafisa wakuu wa Urusi wamewekewa vikwazo na Marekani kutokana na masuala tofauti ikiwa ni pamoja na mzozo wa Crimea nchini Ukraine hadi madai ya Urusi kuingilia uchaguzi Marekani.
Kwa upande mwingine, wanajeshi wawili wa zamani wa Marekani sasa wako katika magereza ya Urusi, wakituhumiwa kwa ujasusi.

