Matokeo ya Tuzo za BET yalivyopokelewa Tanzania

0
Diamond Platnumz

Hisia mbalimbali zimeanza kutolewa mitandaoni nchini Tanzania baada ya ushindi wa mwanamuziki wa Nigeria Burna boy katika tuzo za BET .

Damini Ebunoluwa Ogulu maarufu Burna boy aliwashinda wapinzani wake wakuu katika tuzo hiyo ya kimataifa wanamuziki Naseeb Abdul Juma wa Tanzania maarufu Diamond Platinumz na Wizkid kutoka Nigeria.

Na punde tu baada ya tuzo hizo kutangazwa baadhi ya Watanzania waliokuwa wakiendesha kampeni ya pingamizi dhidi ya Diamond mtandaoni wakiwa na lengo la mwanamuziki huyo kuondolewa katika tuzo hizo walifurahi.

Mmoja ya waanzilishi wa kampeni hiyo na wanaharakati wa haki za kibinadamu nchini humo Maria Sarungi aliandika :

‘’Asanteni sana ❤️ wapendwa!

Mtu asikwambie kuwa sauti yako haina nguvu!

Wakati tunaanza najua watawala walitubeza, kama kutukana tumetukanwa lakini hamkukata tamaa

Sasa tuendelee kudai HAKI na Uwajibikaji kwa enablers and collaborators wote ✊’’

Badala yake Bi Sarungi alimpongeza mshindi wa Tuzo hiyo Burnaboy.

hatahivyo kuna wale waliokuwa wakimpigia Debe Diamond Platinumz kushinda tuzo hiyo, waliodai kwamba wale walioanzisha kampeni hiyo hawakuwa na uzalendo.

Msemaji wa serikali ya Tanzania Gerison Msigwa hakuwachwa nyuma katika mjadala huo ambapo amempongeza Diamond kwa kuwakilisha taifa hilo, akisema kwamba licha ya msanii huyo kutofauti alileta heshima kubwa kwa Tanzania.

Aliandika katika mtandao wa Twitter akisema: ‘’Watanzania tunajua wewe ni Mshindi, Mpambanaji, Mzalendo wa kweli na Mwanamuziki bora sana Afrika na Duniani. Tutaipata wakati mwingine’’.

Diamond akitoa shukran zake za dhati kwa wale waliomuunga mkono kwa dhati akisema kwamba kupitia tuzo hiyo ameoana upendo na umoja wa Watanzania.

Aliongezea kwamba ni faraja kuona Dunia inapotaja nchi zenye Wanamuziki bora Tanzania inatajwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable