Ndejembi akabidhi mifuko 1136 ya Saruji kusaidia sekta ya elimu jimboni kwake

0

KATIKA kuhakikisha anaimarisha sekta ya elimu na afya katika Jimbo lake la Chamwino Mkoani Dodoma, Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi ambaye pia ni Mbunge wa Chamwino amekabidhi vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya Sh Milioni 20.

Naibu Waziri Ndejembi amekabidhi vifaa hivyo leo katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chamwino ambapo amewataka watendaji wa kata ambao wataenda kusimamia ujenzi kwenye maeneo yao kutumia vifaa hivyo kwa weledi na kama ilivyokusudiwa.

Vifaa ambavyo vimetolewa leo na Naibu Waziri Ndejembi ni Mifuko 1136 na Bati 50 ambavyo vyote vinaenda kutumika katika vijiji mbalimbali vilivyopo Jimbo la Chamwino.

" Lengo langu tangu awali nilisema nataka kuona sekta ya elimu inapiga hatua, hili ni Jimbo ambalo Ikulu ipo ni lazima maendeleo yetu ya kielimu yafanane na Ikulu, vifaa hivi navyotoa leo vikawe chachu kwa ufaulu wa wanafunzi wetu kuongezeka.

Nimetoa Mifuko ya Saruji 1136 na Bati 50 ambavyo vyote thamani yake ni Sh Milioni 20, lakini pia nimekabidhi Sh Milioni Tatu kwa ajili ya kuboresha kilimo cha Zabibu Chinangali na Sh Milioni Moja na Nusu kwa ajili ya ununuzi wa magodoro Shule ya Msingi Buigiri Blind," Amesema Ndejembi.

Amewataka watendaji wa kata 13 ambazo zitanufaika na vifaa na michango hiyo kusimamia utekelezaji wake vizuri huku pia akiwasisitiza madiwani na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi CCM kuwa wakali wanapoona vifaa hivyo vinatumika vibaya.

Huu ni muendelezo wa Naibu Waziri Ndejembi kutekeleza ahadi zake alizozitoa wakati wa kampeni katika eneo la Elimu ambapo awali Februari mwaka huu alikabidhi kiasi cha Sh Milioni 19 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya sekta ya elimu Jimboni humo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable