Patrick Vieira kutua Crystal Palace

0

MKATA umeme na nahodha wa zamani wa klabu ya Arsenal, Patrick Vieira yupo kwenye mazungumzo na klabu ya Crystal Palace ili kuchukua nafasi ya Roy Hodgson kama kocha mpya wa timu hiyo.

Inaelezwa kuwa mpaka sasa tayari mazungmzo ya pande hizo mbili yamekamilika kwa asilimia 75.

Palace wamefikia maamuzi hayo baada ya kushindwana na kocha, Nuno Espirito Santo, huku ofa yao kwa  kocha Lucien Favre ikipigwa chini mapema mwezi huu.

Vieira, ambaye alifutwa kazi na klabu ya Nice mwezi Desemba mwaka jana, anatajwa pia kuchukua majukumu ndani ya kikosi cha Selhurst Park.

Kwa sasa nyota huyo wa zamani wa Arsenal anafanya kazi kama mchambuzi wa soka katika kituo cha ITV cha Uingereza kama mchambuzi wa michuano ya Euro 2020.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable