Pendekezo la sheria inayoruhusu ndoa ya mwanamke kuolewa na wanaume wengi lazua hisia Afrika kusini

0
Ndoa ya mwanamke mmoja kuolewa na wanaume wengi

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Ndoa ya mwanamke mmoja kuolewa na wanaume wengi

Pendekezo la Afrika Kusini kuhalalisha ndoa ya mke mmoja aliye na wanaume wengi kwa wakati mmoja imezua hisia kali na kupingwa na wengi miongoni mwa wahafidhina nchini humo.

Hatua hiyo haimshangazi Profesa Collins Machoko, msomi maarufu kuhusu suala hilo.

''Pingamizi hizo ni kuhusu 'udhibiti ', aliambia BBC.

Jamii ya Kiafrika haipo tayari kwa usawa kamili. Hatujui tuwafanyie nini wanawake ambao hatuwezi kuwadhibiti.

Afrika Kusini ina mojawapo ya katiba zilizo na uhuru mkubwa duniani , inayounga mkono ndoa za jinsia moja na ndoa ya mwanamume kuoa wake wengi..

Mfanyabiashara na mtangazaji wa runinga Musa Mseleku ambaye ana wake wane ni kati ya wale wanaopinga ndoa ya mwanamke kuolewa na wanaume wengi.

"Hii itaharibu tamaduni za Kiafrika . Je watoto wa wanaume hao? Je watatambulika vipi? aliuliza bwana Mseleku.

"Wanawake hawawezi kuchukua jukumu la mwanamume. Haijasikika. Je wanawake sasa watalipa mahari kumuoa mwanamume?. Je Mwanamume atahitajika kuchukua jina la mwanamke kama jina lake la pili?.

Ndoa za siri

Prof Machoko alifanyia utafiti ndoa ya mwanamke kuoa wanaume wengi katika taifa lake la kuzaliwa linalopakana na Zimbabwe.

Alizungumza na wanawake 20 na wanaume 45 walioshiriki katika ndoa kama hizo , licha ya kwamba ni kinyume na utamaduni na kwamba hazitambuliki kisheria.

''Ndoa ya mwanamke kuolewa na wanawake wengi zimeepukwa na baadhi ya jamii . Siri ni sawa na ile inayopatikana katika Wamasoni'', alisema.

''Wanapoulizwa na mtu wasiemuamini ama wasiyemjua , hukana kwamba ndoa kama hiyo haipo''.

Haya yote yanatokana na hofu ya athari za baadaye.

"Mke mmoja aliunga mkono wazo la kutaka kuwa wanaume wengi wakati alipokuwa katika darasa la sita akiwa na umri wa miaka 12 baada ya kufahamu jinsi nyuki mama katika mzinga wa nyuki anavyoishi na nyuki wengi wanaume'' , Professa huyo alisema.

Nyota wa kipindi cha ndoa ya wanawake wengi Musa Mseleku

CHANZO CHA PICHA,MUSA MSELEKU

Maelezo ya picha,

Nyota wa kipindi cha ndoa ya wanawake wengi Musa Mseleku

Wakati alipokuwa mtu mzima alianza kushiriki ngono na wanaume tofauti ambao walikuwa wanajuana.

Wanaume wanne kati ya tisa walikuwa katika kundi la kwanza la wavulana aliokuwa katika uhusiano nao.

Katika ndoa kama hiyo mwanamume ndiye huwasilisha ombi la uhusiano huo na kuwaalika wanaume wenza kujiunga na ndoa yake.

Wengine hulipa mahari na wengine hutaka kuchangia jinsi watakavyoishi.

Mwanamke huyo ana uwezo wa kumpatia talaka mwanamume wake mmoja ambaye anafikiri anayumbisha uhusiano wake na wanaume wengine.

Profes Machoko anasema penzi ndio sababu kuu ya wanaume aliowahoji ambao walisema walikubali kuwa wanaume wenza.

Hawakutaka kuhataraisha kumpoteza mke wao.

Baadhi ya wanaume pia walisema kwamba hawakumtosheleza mke wao katika tendo la ndoa, na kwamba wanakubali mpango wa wanaume wenza ili kuzuia kupata talaka ama mahusiano mengine.

Suala jingine ni la kushindwa kupata Watoto.

Baadhi ya wanaume walikubali wake zao kuolewa na wanaume wenza ili kupata watoto.

Kwa kufanya hivyo wanaume huokoa sifa zao kwa umma na kuzuia unyanyapaa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable