Pigano la Mayweather na Logan Paul lamalizika bila mshindi

0

 Pigano la Mayweather na Logan Paul lamalizika bila mshindi

Floyd Mayweather Jr V Logan Paul

Mbabe wa masumbwi Floyd Mayweather Jr amekutana na kisiki asichokitarajia cha Logan Paul katika pambano la ndondi la kujiburudisha lilimalizika bila kupatikana mshindi.

Paul, ambaye ni maarufu kwenye mtandao wa YouTube ameonyesha upinzani mkali katika pambano hilo la raundi nane dhidi ya Mayweather ambaye hajawahi kupoteza mchezo wowote kati ya michezo yake 50 ya ndondi aliyopigana.

Kabla ya pambano hilo, Mayweather na Paul walieleza kwamba wanataka kutoa burudani ya kweli kwa wote wataotazama.

Floyd Mayweather Jr V Logan Paul

Utofauti wa uzoefu na uwezo katika masumbwi kati ya Mayweather na Paul, uliwafanya wengi kuamini kwamba Paul angegaragazwa mapema tu kwa Knock out, lakini Paul alioyesha kwamba si mshawishi tu bali hata kwenye ulingo wa masumbwi.

Mayweather ambaye kama angetumia nguvu zake na uwezo wake wa kawaida basi angemshinda kirahisi Paul mapema tu, lakini alimsukumia makonde ya kawaida mpinzani wake huyo.

Pambano hilo halikuwa la ushindani, lilikuwa la maonyesho na hakutangazwa mshindi kwa kuwa halikuwa na jaji.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable