Sababu DPP kuwafutia kesi viongozi wa Uamsho

0


Dar es Salaam. Miaka saba baada ya viongozi 36 wa Jumuiya za Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) kusota gerezani wakiwa mahabusu, hatimaye wamerejea nyumbani baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuwafutia kesi hiyo huku akibainisha sababu kubwa kufikia uamuzi huo ni udhaifu wa ushahidi.

Viongozi hao wa Uamsho waliachiliwa huru kutoka mahabusu kuanzia juzi usiku, baada ya DPP kuwafutia kesi ya ugaidi iliyokuwa ikiwakabili.

Hadi wanaachiliwa huru juzi, viongozi hao walikuwa wameshakaa mahabusu kwa miaka saba kutokana na kukabiliwa na mashtaka hayo ambayo ni miongoni mwa makosa yasiyo na dhamana kwa mujibu wa sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA).

Kwa muda mrefu, wadau na wanaharakati mbalimbali walikuwa wakipaza sauti za kutaka viongozi hao waachiwe, kutokana na kukaa muda mrefu bila kesi yao kusikilizwa, huku Serikali ikieleza kuwa kuchelewa kusikilizwa kulikuwa kunatokana na kuchelewa kukamilika kwa upelelezi, ambao ulikuwa unafanyika mpaka nje ya mipaka ya nchi.

Hata hivyo, uamuzi huo wa DPP kuwafutia kesi hiyo umekuja wakati tayari kesi hiyo ikiwa imeshaanza kusikilizwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, baada ya upelelezi wake kukamilika.

Lakini, uamuzi huo pia umekuja siku chache baada ya Mahakama Kuu kuwafutia jumla ya mashtaka 14 katika ya mashtaka 25 yaliyokuwa yakiwakabili na hivyo kuwabakizia mashtaka 11 tu, huku Serikali ikikata rufaa Mahakama ya Rufani kupinga amuzi huo wa Mahakama Kuu kuwafutia mashtaka hayo bila mafanikio.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable