Serikali ya Marekani kupitia Ubalozi wake wa Tanzania imetangaza kwamba itanunua dozi milioni 500 za chanjo ya COVID-19 aina ya Pfizer COVID-19 na kuzitoa msaada kwa Nchi mia moja (100) zenye kipato cha chini duniani.
Taarifa hiyo ya Ubalozi wa Marekani Nchini Tanzania imesema "Hii ni ahadi na msaada mkubwa unaotolewa na Watu wa Marekani kuwasaidia Watu duniani kote"
Mpaka sasa covid-19 imesababisha vifo vya Watu milioni 3.78 huku Wagonjwa wakifikia milioni mia moja sabini na tano.
