Serikali yatoa agizo zito kwa watumishi waliokwapua Mil 83 wilayani Makete

0


Na Amiri Kilagalila,Njombe

Serikali mkoani Njombe imeagiza kurejeshwa kwa fedha kiasi cha shilingi milioni 83 zinazodaiwa kukwapuliwa na baadhi ya watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Makete na kusababisha hoja za mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali  CAG

Duru zinaarifu kuwa baada ya wizi huo baadhi ya watumishi walitokomea kusiko julikana kwa kuhofia kutiwa nguvuni na hatimaye korokoroni ambapo mkuu wa  mkoa wa Njombe mhandisi Marwa Rubirya amemuagiza mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Makete   Francis Namaumbo kuhakikisha  fedha hizo  zinarejeshwa haraka iwezekanavyo.

Maagizo  hayo ameyatoa katika baraza maalumu la kupitia hoja za mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG wilayani Makete na kwamba hakuna mtumishi atakayesalia salama ilihali ni mwizi.

“Baadhi ya watumishi wanaondoka na fedha lakini jitihada zinazotumika kurejesha fedha hizo bado ni kidogo,kwa hiyo nitoe maelekezo kuhakikisha wote walioshiriki kuondoka na fedha zilizotakiwa kuwasilishwa benki,mwisho wa mwezi huu ziwe zimerejeshwa na taarifa iwasilishwe kwa katibu tawala wa mkoa”alisema Rubirya

Licha ya halmashauri ya wilaya ya makete kupata hati safi lakini ametaka kurekebisha mapungufu yanayosababisha kuwapo kwa hoja za mkaguzi.

“Kama alivyosema mkaguzi wan je kupata hati safi si kazi ndogo ni kazi kubwa lakini hii imetokana na ushirikiano ambao watendaji wamekuwa nao na mtendaji wa halmasahauri lakini tuepuke hizo hoja ambazo zimekuwa zikijirudia”aliongeza Rubiry

Baadhi ya madiwani waliozungumza na kituo hiki akiwemo Atilio   Ng'onda wamesema  ushirikiano baina yao na  mkurugenzi wa halmashauri hiyo pamoja na watumishi ndio sababu ya  kupata hati safi huku wakieleza ni kwa nini baadhi ya watumishi wameendelea na tabia ya kukimbia na mapato ya serikali.

“Waliokimbia na mali za halmashauri nafikiri kuna mipango mkakati ambao sasa vyomba vyetu vya halmashauri vinakwenda kulisimamia hili kwa haraka ili kuona hi fedha inarudi na hata mkuu wa mkoa amesema lazima hizo fedha zirejeshwe”alisema Atilio   Ng'onda

kumeripotiwa mapungufu ya kuwapo kwa hoja za mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali CAG katika halmashauri mbalimbali hapa nchini hatua ambayo imesababisha kutolewa kwa maagizo mazito kwa baadhi ya maofisa wa serikali wanaotuhumiwa kuhusika katika ripoti hizo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable