Spika wa zamani wa Iran adai maelezo ya kunyimwa kushiriki uchaguzi Mkuu

0



Spika wa zamani wa Bunge la Iran Ali Larijani ametaka kupewa maelezo kutoka kwa tume ya uchaguzi juu ya sababu ya kunyimwa nafasi ya kushiriki katika uchaguzi Mkuu wiki ijayo. Mwezi uliopita tume hiyo iliwaidhinisha wagombea saba pekee kushiriki uchaguzi huo wa siku ya Ijumaa na kuwanyima nafasi hiyo wagombea mashuhuri akiwemo Larijani na aliyekuwa rais wa Jamhuri hiyo ya kiislamu Mahmoud Ahmadinejad. Hatua hiyo ya kuwanyima fursa ya kushiriki wagombea mashuhuri nchini humo itaongeza uwezekano wa kuibuka mshindi Jaji Mkuu wa Iran Ebrahim Raisi, ambaye ni mshirika wa kiongozi wa juu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable