Everton wanataka kumsaini nyota wa Wolves na England Conor Coady mwenye umri wa miaka 28.(Football Insider)
Chelsea wanataka kujenga uhusiano mzuri na Borussia Dortmund kwani wanatarajia kusaini wachezaji wao wawili bora zaidi - mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland, 20, na kiungo wa kati wa Uingereza 17 Budaham (Star)
Manchester United wamepata ombi la kufungua ofa ya pauni milioni 50 kwa beki wa Real Madrid na Ufaransa Raphael Varane, lakini Real wanataka pauni milioni 80 kwa mchezaji huyo wa miaka 28(Manchester Evening News)
Walakini, kuondoka kwa Sergio Ramos kutoka Real kunaweza kudhoofisha mipango ya United ya kumsajili Varane baada ya wababe hao wa Uhispania kufungua mazungumzo ya mkataba mpya na beki huyo wa kati. (Times)
Mlinzi wa Morocco mwenye umri wa miaka 22, anayeichezea Inter Milan Achraf Hakimi "amekubali kwa ahadi ya mdomo" kujiunga na Chelsea. Mabingwa wa Italia, ambao tayari wamekataa maombi ya ununuzi ya nyota huyo kutoka kwa Blues na Paris St-Germain, wanaripotiwa kutaka pauni milioni 43 pamoja na beki wa kushoto wa Uhispania wa Chelsea, Marcos Alonso, 30 (Ekram Konur via Sun)
PSG wanajiandaa kuweka mezani ombi la pili kwa Hakimi la euro 70m (Pauni milioni 60). (Footmercato - in Italian)
Roma watajaribu kumsajili kiungo wa Aston Villa na Brazil Douglas Luiz, 23, ikiwa watashindwa kumpata kiungo wa Arsenal na Uswizi Granit Xhaka, 28. (Gazzetta dello Sport - in Italian)
Crystal Palace wamefanya mawasiliano na mwakilishi wa meneja wa zamani wa Borussia Dortmund Lucien Favre wakati wanaendelea na utaftaji wa meneja mpya. (Guardian)
Albert Lokonga, 21 wa klabu ya Anderlecht na kipa wa Sheffield United na England Aaron Ramsdale, 23, ni miongoni mwa wachezaji wanaolengwa na Arsenal wakati Mikel Arteta anaonekana kurekebisha kikosi chake. Kiungo wa kati wa Ubelgiji Lokonga anasemekana kuwa na thamani ya pauni milioni 17.5 (Goal)
Leicester City wanatumai Youri Tielemans, 24, atasaini kandarasi mpya na kilabu hiyo huku kukiwa na uvumi kuhusu hatima yake . Kiungo huyo wa Ubelgiji amekuwa akihusishwa na Manchester United na Liverpool. (Leicester Mercury)
Leicester City wameongeza nia yao ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa RB Salzburg na Zambia Patson Daka, 22. (Telegraph)
Eriksen kuwekewa kifaa maalumu kwenye moyo
Kiungo anayecheza kwa mkopo huko West Ham Jesse Lingard, 28, anatarajiwa kufanya mazungumzo na Manchester United juu ya hatma yake atakaporudi kwa mazoezi ya kujiandaa kwa msimu ujao mwezi Jumai ikimaanisha the hammers lazima wasubiri kujua ikiwa wanaweza kumsaini mchezaji huyo wa England kabisa. (Star)
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp anafuatilia hali ya mshambuliaji wa Real Sociedad na Sweden Alexander Isak. Mchezaji huyo wa miaka 21 alifunga mabao 17 kwenye La Liga msimu uliopita na kuisaidia La Real kushinda Kombe la Copa del Rey (Express)
Brighton wamefeli kwenye kikwazo cha mwisho katika harakati za kumsajili mshambuliaji wa Stuttgart Nicolas Gonzalez. Seagulls walikuwa wamekubali ada ya rekodi ya kilabu ya karibu pauni milioni 25 pamoja na mafao ya mchezaji huyo wa miaka 23 lakini Muargentina huyo anaonekana ameamua kujiunga na Fiorentina ya Italia badala yake(Sky Germany, via Team Talk)
