Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 17.06.2021: Ramos, White, Odegaard, Lamptey, Welbeck, Trippier

0
Ramos

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Nahodha anayetimka Real Madrid Sergio Ramos, huenda akatua katika moja ya vilabu vya Paris St-Germain, Manchester City, Manchester United na Sevilla. Mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 35, aliyeanzia maisha yake ya soka Sevilla, anaondoka Real baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miaka 16 kufutia kushindwa kuafikiana kuhusu kuongeza mkataba mpya. (AS - in Spanish)

Brighton imekataa dau la £40m kutoka Arsenal kwa ajili ya mlinzi wa England Ben White (23). Mlinzi huyo ameicheza Brighton mechi 36 za ligi kuu England msimu uliopita na kufanikiwa kuitwa timu ya taifa ya England mwezi May, mwaka huu. (Sky Sports)

Martin Odegaard

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Arsenal wamerudi nyuma kuhusu mpango wao wa kumsajili nyota wa kimataifa wa Norway Martin Odegaard, 22, ambapo kiungo huyo anatarajiwa kusalia klabuni kwake Real Madrid baada ya kutumia sehemu ya pili ya msimu akiwa kwa mkopo Emirates. (AS - in Spanish)

Winga wa Ufaransa Kingsley Coman, 25, anataka kuhamia ligi kuu ya England baada ya kugoma kusaini mkataba mpya Bayern Munich. (Sky Sports)

Inter Milan inajiaandaa kupambana na Everton katika mbio za kusaka saini ya mlinzi wa Uholanzi, Denzel Dumfries, 25, kutoka PSV Eindhoven. (Voetbal International - in Dutch)

Brighton imekubaliana na Stuttgart katika uhamisho ulioweka rekodi kwenye klabu hiyo wa £25m kwa ajili ya mshambuliaji muargentina Nicolas Gonzalez, 23, ambaye amepachika mabao 6 katika michezo 15 ya ligi kuu ya Ujerumami msimu wa 2020-21. (Guardian)

Tottenham wanamtaka mlinzi wa kulia wa Brighton na timu ya taifa ya England chini ya miaka 21 Tariq Lamptey, 20, ambaye ameng'ara msimu uliopita akiwa na kikosi cha Graham Potter, kabla ya kupata majeraha mwezi Desemba yaliyomuweka nje ya uwanja mpaka mwisho wa msimu. (Sky Sports)

Brighton pia wako kwenye mazungumzo na nyota wa zamani wa England Danny Welbeck, 30 kuhusu mkataba mpya. (The Argus)

Danny

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Matumaini ya mshambuliaji wa England Harry Kane, ya kutimka Tottenham kuelekea kwa mabingwa wa ligi kuu England Manchester City yanakutana na ugumu kufuatia vilabu hivyo kupangwa kucheza mechi ya kufungua pazia la ligi kuu 2021-22. (The Telegraph - subscription required)

Sheffield United huenda ikalazimika kukubali dau la Arsenal kwa ajili ya kiungo wake kutoka Norway Sander Berge. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 anasema anamatumaini kwamba atacheza ligi ya mabingwa Ulaya msimu ujao. (Sheffield Star)

Leeds haijakata tamaa ya kumshawishi Ezgjan Alioski,29, kuendelea kusalia Elland Road. Winga huyo wa Macedonia anatarajia kutimka kama mchezaji huru msimu huu baada ya kushindwa kuafikiana kuhusu mkataba mpya, akionekana kupunga mkono wa kwaheri katika siku ya mwisho ya msimu. (Mirror)

Crystal Palace wanatarajiwa kuzungumza na kocha wa zamani wa Borussia Dortmund Lucien Favre wakati huu wakiendelea na harakati zao za kusaka kocha mpya. (Sun)

Kieran Trippier started at left-back in England's Euro 2020 Group D win over Croatia

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Dau la kwanza la Manchester United kwa ajili ya mlinzi wa pembeni Kieran Trippier limekataliwa na Atletico Madrid. Mabingwa hao wa La Liga wanataka angalau dau hilo likaribie £35m kumruhusu muingereza huyo mwenye umri wa miaka 30. (Guardian)

Chelsea imepeleka dau la £51.5m pamoja na kumtoa Marcos Alonso kwa ajili ya kumnasa mlinzi wa pembeni wa Inter Milan raia wa Morroco Achraf Hakimi, 22, ambaye anasakwa pia na klabu ya Paris St-Germain. (La Repubblica - in Italian)

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable