Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 24.06.2021: Messi, Kane, Rodriguez, Nuno, Ramos, Hakimi, Gilmour, Smith Rowe

0
Lionel Messi

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Mshambuliaji nyota wa Argentina Lionel Messi, 33, bado hajafanya uamuzi iwapo atasalia Barcelona au la, akiwa amebaki na wiki moja kumaliza mkataba wake na klabu hiyo ya Uhispania. (Marca)

Tottenham wanapanga kufanya mazungumzo na mkufunzi wa zamani wa Wolves Nuno Espirito Santo kuhusu mpango wa kuchukua nafasi ya ukocha, baada ya awali kumuacha nje ya kinyang'anyiro Mreno huyo mwenye miaka 47. (Football Insider)

Manchester City wako tayari kusubiri kwa mwaka mmoja kumpata mshambuliaji endapo juhudi zao za kumsajili mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane, 27, kutoka Tottenham msimu huu wa joto zitagonga mwamba. (ESPN)

Harry Kane

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane

Wawakilishi wa kiungo mshambuliaji wa Everton James Rodriguez wamemnadi mchezaji huyo kwa klabu kubwa za Ulaya Real Madrid, Atletico Madrid, AC Milan na Napoli baada ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Colombia aliye na umri wa miaka 29 kuonesha yuko tayari kuondoka uwanja wa Goodison Park club. (Mail)

Paris St-Germain wamewasilaiana na kiungo wa kati wa Uhispania Sergio Ramos ,35, ambaye mkataba wake na Real Madrid unamaliza mwisho wa mwezi huu. (Goal)

Achraf Hakimi

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

PSG wafikia mkataba na Inter Milan kuhusu usajili wa Achraf Hakimi

PSG wameafikiana na Inter Milan kumsaini winga wa Morocco Achraf Hakimi kutoka klabu hiyo ya Serie A kwa kima cha euro milioni 59.8, ikijumuisha marupurupu ya ziada. (ESPN)

Arsenal wanaamini watafanikiwa kumshawishi kiungo wa kati Muingereza Emile Smith Rowe,20, kusaini mkataba mpya licha ya Aston Villa kuonesha nia ya kutaka kumnunua. (Football London)

Emile Smith Rowe,20,

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Arsenal kumshawishi kiungo wa kati Emile Smith Rowe asiondoke

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amevutiwa na mchezo wa kiungo wa kati wa Aston Villa na Scotland John McGinn, lakini itahitaji kati ya pauni milioni 45-50 kumshawishi mchezaji huyo wa miaka 26 kundoka Villa Park. (The Athletic - subscription required)

Mchezaji wa Manchester United wa safu ya uinzi Axel Tuanzebe,23, anatarajiwa kuondoka klabu hiyo kwa mkopo msimu huu wa joto. (Manchester Evening News)

Ryan Bertrand

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Mlinzi wa Southampton Ryan Bertrand

Muingereza Ryan Bertrand, 31, anayecheza safu ya ulinzi anajiandaa kujiunga na Leicester City kwa uhamisho wa bure mwanzo wa Julai hadi mwisho wa mkataba wake na Southampton. (Goal)

Wolves wanamtaka mchezaji wa kimataifa wa Uskochi Billy Gilmour, 20, kwa mkataba wa bila malipo kutoka Chelsea. (Football Insider)

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable