Tetesi za soka Ulaya Jumanne 29.06.2021: Ramos, Bale, Camavinga, Patricio, Belotti, Gilmour, Greenwood

0
Sergio Ramos

CHANZO CHA PICHA,EPA

Beki wa Uhispania Sergio Ramos ,35, anachunguza maombi aliyopata kutoka kwa Manchester City , PSG na Bayern Munich kabla ya kufanya uamuzi kuhusu hatma yake. (ESPN)

Tottenham Hotspur haina mbadala wa kuongeza kandarasi ya mkopo na mchezaji Gareth Bale 31, kwa msimu wa pili na mchezaji huyo anatarajiwa kurudi katika klabu yake ya Real Madrid , ambapo amesalia na kandarasi ya miezi 12 .. (Evening Standard)

Rennes inasema kwamba haijapata ombi lolote la kiungo wa kati na raia wa Ufaransa Eduardo Camavinga, licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 kuhusishwa na klabu ya Manchester United na PSG. (Metro)

Eduardo Camavinga

CHANZO CHA PICHA,REUTERS

Roma inakaribia kukubali kuweka mkataba na kipa wa Portugal Rui Patricio, 33 kutoka Wolves.. (Sky Sports)

Arsenal inamnyatia mshambuliaji wa Torino na Itali Andrea Belotti, lakini AC Milan, Fiorentina, Napoli na Roma zote zinamchunguza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka. (Tuttosport, via 90Min)

Mshambuliaji wa Inter Milan na Uruguay Martin Satriano, 20, anavutia hamu kutoka kwa klabu za Arsenal, Everton, Tottenham na Everton. (Mail)

Leicester City ni miongoni mwa klabu kadhaa zinazomtaka mshambuliaji wa Itali Domenico Berardi , anayeichezea klabu ya Sassuolo mwisho wa msimu ujao (Gazzetta Dello Sport, via Leicester Mercury)

Andrea Berlotti

CHANZO CHA PICHA,REUTERS

Norwich City inakaribia kumsaini kwa mkopo kiungo wa kati wa Scotland Billy Gilmour, 20 kutoka Chelsea (Sky Sports)

Liverpool huenda ikamsaini mshambuliaji wa Porto na Brazil Otavio, 26, kabla ya siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho siku ya Jumatano kutokana na kifungo kinachomzuia cha £34m. (Star)

Aston Villa na Norwich zote zinajaribu kumsaini kipa wa England mwenye umri wa miaka 18 Matthew Cox kutoka klabu ya daraja la kwanza AFC Wimbledon. (Football Insider)

Barcelona inafikiria kumpatia kandarasi ya miaka miwili beki wa Uhispania mwenye umri wa miaka 29 Sergi Roberto , ambaye mkataba kwake unakamilika 2022. (Marca)

Serfi Robero

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

West Ham United huenda ikamuajiri Alan Irvine, ambaye alikuwa msaidizi wa mkufunzi wa West Ham David Moyes, kuwa mkurugenzi wa kandanda katika klabu hiyo. (Football Insider)

Barnsley ipo katika mazungumzo na mkufunzi wa klabu ya TSV Hartberg , Markus Schopp kuhusu uwezekano wa kocha huyo wa Austria kuwa mkufunzi mpya kutokana na kuondoka kwa Valerien Ismael kuelekea West Bromwich Albion. (Sky Sports)

Jamaica inamtaka mshambuliaji wa Manchester United Mason Greenwood, 19, kubadilisha uraia wake kutoka England . Wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 ambao hawajachezea taifa hilo mechi tatu kubwa wana uwezo wa kufanya mabadiliko kama hayo.. (Telegraph - subscription required)

TETESI ZA JUMATATU

Antoine Griezman

CHANZO CHA PICHA,EPA

Manchester City huenda wakamlenga mshambuliaji wa Barcelona na Ufaransa Antoine Griezman , 30 kama mbadala wa mshambuliaji wa England na Tottenham Harry Kane.(Fichajes, in Spanish)

Manchester United imempatia Jesse Lingard kandarasi mpya ya miaka mitatu huku kiungo huyo wa England akiwavutia West Ham. (Mirror)

Liverpool ina hamu ya kumsaini mshambuliaji wa Bayern Munich na Ufaransa Kingsley Coman na inawasiliana na usimamizi wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (Sport 1 via Metro)

Inter Milan wamewasiliana na wakala wa beki wa kulia wa Arsenal Hector Baellerin huku klabu hiyo ya Itali ikimlenga mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 raia wa Uhispania atakayechukua mahala pake Achraf Hakimi. (Gianluca di Marzio, in Itali.

Hakimi Achraf

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Kiungo wa kati wa Arsenal na Switzerland Granit Xhaka amethibitisha kuondoka katika klabu hiyo ya ligi ya premia kuelekea AS Roma wakati wa mkutano wa kombe la Euro 2020.. (90 min)

Manchester United wanakutana na wakala wa kiungo wa kati wa Rennes 18, Eduardo Camavinga wiki ijayo kuandikisha kandarasi. (RMC, via Mirror)

Kiungo wa kati wa West Ham Felipe Anderson huenda akarudi Lazio baada ya klabu hiyo kuanzisha mazungumzo ya kumsajili mchezaji huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 28.. (Mail)

Felippe Anderson

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Klabu ya Borussia Dortmund itamlenga mshambuliaji wa PSV Eindhoven na England Noni Madueke, 19, kuchukua nafasi itakayowachwa wazi na Jadon Sancho ambaye anatarajiwa kutia saini kandarasi ya dau la £77m na klabu ya Manchester United . (Ruhr Nachrichten, in German)

Southampton inakaribia kukamilisha kumsaini beki wa klabu ya Brests na Ufaransa Romain Perraud, 23, na pia wana hamu ya mshambuliaji wa Blackburn Rovers Adam Armstrong ,24. (Athletic, subscription required)

Miaka miwili baada ya kukataa kujiunga na Arsenal, kiungo wa kati wa Leicester na Ubelgiji Dennis Praett 27, huenda akasajiliwa na klabu hiyo katika dirisha hili la uhamisho. (Express)

Dennis Praet

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Beki wa Brighton na England Ben White, 23, anasema kwamba hajui kile ambacho ni kweli kuhusu uvumi kwamba anaelekea kujiunga na Arsenal kwa dau la £50m. (TalkSport)

Arsenal wameonesha hamu ya kumsajili kiungo wa kati wa lille na Portugal Renato Sanchez na wameitaka klabu hiyo ya Ufaransa kuipatia habari zozote kumuhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23.. (90 min)

Liverpool imekataa ombi la klabu ya Uswizi ya FC Basel kumnunua mshambuliaji wa Canada mwenye umri wa miaka 21- Liam Millar na inataka kulipwa fedha za ziada za £1m ili kumuuza mshambuliaji huyo.* (Goal)

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable