Jadon Sancho atapokea mshahara wa £250,000 kwa wiki iwapo atakamilisha uhamisho wa kuelekea Manchester United , ikiwa ni zaidi ya mara 2 ya mshahara ambao winga huyo wa England anapokea katika klabu ya Borussia Dortmund kwa sasa. (Star)
Mshambuliaji wa Inter Milan Romelu Lukaku amesema kuna uwezekano wa yeye kurudi katika ligi ya Premia mbali na kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 amehusishwa na kumrithi Robert Lewandowsky katika klabu ya Bayern.. (Mirror)
Liverpool imeuliza kuhusu uwepo wa mshambuliaji wa PSG na Ufaransa Kylian Mbape , 22 ambaye pia amehusishwa na uhamisho wa Real Madrid . Kandarasi ya Mbappe katika klabu ya PSG inakamilika 2022.. (Marca)
Mshambuliaji wa Inter Milan Romelu Lukaku amesema kuna uwezekano wa yeye kurudi katika ligi ya Premia mbali na kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 amehusishwa na kumrithi Robert Lewandowsky katika klabu ya Bayern.. (Mirror)
Real Madrid inajiandaa kuwasilisha ombi la kuwasajili beki wa Leicester City na Ufaransa Wesley Fofana, 20, pamoja na mwenzake wa Ufaransa Raphael Varane, 28, ambao wanakaribia kujiunga na Manchester United. (Star)
Jadon Sancho atapokea mshahara wa £250,000 kwa wiki iwapo atakamilisha uhamisho wa kuelekea Manchester United , ikiwa ni zaidi ya mara 2 ya mshahara ambao winga huyo wa England anapokea katika klabu ya Borussia Dortmund kwa sasa. (Star)
Dortmund imesema kwamba mshambuliaji wa PSV `na Uholanzi Donyell Malen , 22 ndiye mchezaji atakayechukua mahala pake Sancho iwapo ataondoka katika klabu hiyo. (Mirror)
Manchester City imemuongeza beki winga wa Chelsea na England Reece James katika orodha yake huku mkufunzi Pep Guradiola akisemekana kummezea mate mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21.. (The Athletic - subscription required)
Kiungo machezeshaji wa Barcelona Philippe Coutinho, 29, ana ndoto ya kurudi katika klabu ya Liverpool , lakini The Reds hawana mpango wa kumrudisha raia huyo wa Brazil Anfield.
Mbadala mwengine wa Coutinho ni Kujiunga na Inter Milan au Leicester, ambayo inafunzwa na aliyekuwa kocha wa Liverpool Brendan Rodgers lakini The Foxes wanaataka kumnunu kwa mkopo kwa msimu mmoja.. (Sport - in Spanish)
Aston Villa imejianda kuipatia ushindani Chelsea baada ya kuwasilisha ombi la £40m kumnunua mshambuliaji wa England mwenye umri wa miaka 23 Tammy Abraham, mbaye alifunga magoli 26 katika mechi 40 wakati wa msimu wa 2018-19 akiichezea Aston Villa.
Mshambuliaji wa klabu ya Red Bull Salzburg na raia wa Zambia Patson Daka, 22, anasema kwamba ameamua kujiunga na Leicester baada ya kufunga magoli 34 katika mashindano yote katika msimu wa 2020-21.
Klabu ya Ajax ina hamu ya kumsajili winga wa Tottenham Hotspurs Steven Bergwijn , lakini klabu hiyo ya ligi ya Premia haipo tayari kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 raia wa Uholanzi ambaye alijiunga na Spurs kutoka PSV Eindhoven mwezi Januari 2020. (Mail)
Mkufunzi wa klabu ya Real Madrid Carlo Ancelotti anataka klabu hiyo ya Uhispania kumnunua beki wa Man United na Portugal Diogo Dalot ,22, ambaye alihudumu msimu wa 2020 -21 kwa mkopo akiichezea AC Milan. (Correio de Manha via Sport Witness)
AC Milan ina hamu ya kuwasajili wachezaji watatu wa Chelsea winga wa Morocco Hakim Ziyech, 28, na wachezaji wawili wa Ufaransa Olivier Giroud, 34, na Tiemoue Bakayoko, 26, wote wakinyatiwa. Bakayoko alihudumu msimu wa 2018-19 kwa mkopo akiwachezea mabingwa hao wa Itali. (Di Marzio via Sempre Milan)
Klabu za Leeds United, West Ham na Southampton zote zinamuwania beki wa Barcelona Junior Firpo, 24, huku mchezaji huyo wa Uhispania akitaka kuondoka katika uwanja wa Nou Camp mwisho wa msimu ujao. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Na klabu ya Barcelona itamlenga Marcos Alonso wa Chelsea ,30, iwapo Firpo angeondoka , Ijapokuwa Inter Milan pia inachunguza hali ya beki huyo wa Uhispania katika uwanja wa Stamford Bridge. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Burnley itasikiliza maombi ya beki wa England Jaames Tarkowski, 28, mbaye amehusishwa na uhamisho wa kuelekea West Ham. (Football Insider)





