Tiketi chache kuuzwa kuiona Simba, Yanga


Bodi ya ligi kuu Tanzania TPLB imetoa maelekezo juu ya mashabiki wanaopaswa kukata tiketi, kuzitizama Simba na Yanga katika mchezo wa juni 3 2021 katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kwa mujibu  wa taarifa hiyo jumla ya mashabiki 13,782 ndiyo watakaopaswa kukata tiketi mpya  kwa sababu   katika mchezo uliyohairishwa 8  mei  2021 wale waliokata tiketi kwa mfumo wa NCARD  hawatalazimika kulipa tena.

Mgawanyiko wa tiketi 13,782  kama ufuatavyo tiketi  2,218 ni za jukwaa la kijani ( mzunguko) tiketi 11,280 ni  za jukwaa la machungwa  (orange) na tiketi 284  VIP B taarifa imesisitiza  hakutakuwa na tiketi za VIP A  na C zitakazouzwa  kwa ajili mchezo huo wa julai 3

Viingilio  vimepangwa kama ifuatavyo  mzunguko shilingi 7,000, machungwa  10,000 na   kwa upande wa  VIP B kiingilio ni  20,000

Simba na Yanga wanakutana  baada ya  mchezo wao wa tarehe 8 mei kuhairishwa kufuatia sintofahamu iliyozuka baada ya muda wa mchezo kusogezwa mbele, uwanja wa taifa unachukua mashabiki 60,000

Post a Comment

Previous Post Next Post