Tumeshuhudia kuibuka kwa sarafu mpya zinazotumika kwa njia ya kimtandao

0

 



“Tumeshuhudia kuibuka kwa sarafu mpya zinazotumika kwa njia ya kimtandao najua Nchi nyingi ikiwemo Tanzania hazijakubali au kuanza kuzitumia sarafu hizi hata hivyo wito wangu kwa Bank Kuu ni vema mkaanza kufanyia kazi maendeleo hayo kwa kujitayarisha na kukaa tayari na maendeleo hayo ili yakija yakitukamata yasitukute hatuko tayari”———Rais Samia Suluhu Hassan leo akiwa Mwanza.

“Tunaweza sisi kujiona hatuko tayari lakini Wananchi wetu wakatutangulia wakaanza kuingia huko nje ya Nchi na wakiingia huko bila shaka yatakuja huku kwetu kwahiyo naomba Benki kuu ijiweke tayari, kutokana na utandawazi haitoshangaza Watanzania kututangulia, hivyo ili tusitanguliwe na Wananchi wetu ni vyema tukaanza kujiandaa”
“Pia naiomba Benki Kuu ielekeze nguvu kuhamasisha matumizi kwa njia za mtandao ili kupunguza matumizi ya pesa taslimu, hii sio tu itaongeza usalama wa fedha, bali itarahisisha biashara,ukusanyaji wa mapato na kupunguza uchapishaji wa pesa mara kwa mara”———Rais Samia.
“Naiomba Bank Kuu ihamasishe Taasisi za Fedha ikiwemo Bank ili zitoe mikopo ya muda mrefu, Bank nyingi nchini zinatoa mikopo ya muda mfupi inakuwa vigumu Nchi yetu kukuza sekta za viwanda na kilimo na kuboresha makazi ya Wananchi wetu”———Rais Samia akiwa Mwanza.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable