Uingereza na Australia zaafikiana mikataba ya biashara

0


Uingereza na Australia zimetangaza kufikia mkataba wa biashara huru. Nchi hizo zimekubaliana kuondoa ushuru kwa bidhaa nyingi huku Uingereza ikipania kutanua mashirikiano kote ulimwenguni baada ya kujitoa Umoja wa Ulaya. 


Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, na mwezake wa Australia, Scott Morrison, wameeleza manufaa ya mkataba huo kwa nchi zao na kusisitiza juu ya mahusiano ya muda mrefu baina ya pande hizo mbili. Mkataba wa leo unatarajiwa kuimarisha uuzaji nje ya nchi bidhaa za Uingereza kama vile mvinyo kutoka Scotland, huku ukiongeza pia uagizaji nyama ya kondoo na mvinyo kutoka Australia. 


Uingereza pia inatumai mkataba huo utaisaidia kujiunga na ushirikiano wa kibiashara na nchi za eneo la Pasifiki, hatua ambayo itafungua mlango wa kuongeza biashara katika eneo zima la Asia na Pasifiki. 


Huu ndio mkataba wa kwanza wa kibiashara ambao Uingereza imeutafuta kuanzia mwanzo tangu ilipojitoa Umoja wa Ulaya. Mikataba ya awali na mataifa mengine kama Japan na Canada ilijikita kwenye makubaliano yaliyokuwepo yaliyoafikiwa na Umoja wa Ulaya.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable