Mashindano ya EURO 2020 yanaendelea leo hii kukitarajiwa mechi kali kati ya mabingwa watetezi Ureno na Ubelgiji.
Nahodha wa Ureno Cristiano Ronaldo, anaweza kuweka rekodi ya ufungaji mabao wakati timu yake itakapo ingia ugani katika mechi ya mtoano ya timu 16 bora.
Ronaldo amefikia rekodi ya mabao 109 yaliyofungwa na Ali Daei wa Irani akiwa na magoli 5 katika mashindano haya na anapania kufunga magoli zaidi huko Seville kuisaidia timu yake kusonga mbele katika robo fainali.
Mechi nyengine itakayochezwa leo ni kati ya Uholanzi na Jamuhuri ya Czech.

