Bajeti ya Tanzania iliyowasilishwa hapo jana haijataja wazi kiasi cha fedha kichotengwa kwa ajili ya kukabiliana na janga la Corona.
Mwandishi wa BBC Martha Saranga alizungumza na waziri wa Fedha wa Tanzania Mwigulu Nchemba kuangazia suala hilo .
Shirika la Fedha Duniani (IMF) limethibitisha kwamba litaipatia Tanzania mkopo wa dharura wa takribani dola milioni 574, itakapokamilisha mambo muhimu ikiwemo utoaji wa takwimu kuhusu maambukizi ya virusi vya Corona.
Mara ya mwisho Tanzania kutoa takwimu kuhusu maambukizi ya virusi hivyo na ugonjwa wa Covid 19 kwa ujumla ilikuwa mwezi Mei mwaka 2020.
Mwezi Machi 2020 Serikali ya Tanzania iliiomba IMF mkopo huo wa dharura kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa huo bila mafanikio, kufuatia mazungumzo hayo kuishia njiani. Mwezi Machi mwaka huu, serikali ya Tanzania ilihuisha tena ombi hilo.
Hata hivyo, mwakilishi huyo wa IMF, Reinke amesema bado mchakato ni mrefu kabla ya kuidhinishwa kwa mkopo huo kwa Tanzania, akisema yapo mambo mengi ya kuzingatiwa mbali na utoaji wa takwimu.