Zifahamu faida za kiafya za kulala mchana

0

 



Kuboresha uwezo wako wa kukumbuka

Utafiti una dhihirisha kuwa usingizi unasaidia pakubwa katika kukumbuka matukio. Kulala kunaweza kusaidia kukumbuka mambo uliyo soma siku ikianza sawa na usingizi wa usiku. Kulala kuna kusaidia kuto sahau mambo kama uwezo wa kukumbuka yaliyo semwa na mengine.

Huenda ukaweza kugundua mambo fiche

Kulala hakukusaidii, kukumbuka yaliyo semwa tu. Ila, kutakusaidia ubongo wako kushikanisha mambo na kugundua yaliyo fichwa. Katika somo moja, kulala kuna kusaidia kuelewa mambo uliyo yasikia siku yote.

Kuna boresha ubunifu wako

Mojawapo ya faida za kiafya za kulala zitakazo kushangaza ni kuboresha ubunifu wako. Ushawahi kuamka na fikira bunifu? Dakika 70-90 baada ya kulala, sehemu ya ubongo ina amshwa inayo husika na ubunifu na kuota. Usingizi huu unakusaidia kuleta mawazo pamoja na kupata majibu.

Kuboresha mhemko wako

Ikiwa unahisi hauna raha, jaribu kulala kwa dakika chache kuinua roho na hisia zako. Kulala ama hata kupumzika kwa lisaa limoja kutakusaidia kuhisi vyema. Wataalum wana sema kupumzika kunako tokana na kulala na kupumzika kunasaidia na mhemko wako, ikiwa utalala ama la.

Ungependa kutahadhari na kuwa makini zaidi? Lala

Ukianza kuhisi usingizi baada ya kula chamcha chako, hauko peke yako. Chukua mapumziko ya angalau dakika 20 ulale.

Kulala ni bora ikilinganishwa na kafeini

Ikiwa unahisi kuchoka lakini una kazi ama kusoma ili umalize, unaweza faidika zaidi kutokana na usingizi kuliko kafeini ama kahawa. Ikilinganishwa na kafeini, kulala kunaweza leta makumbusho bora na kusoma.

Faida za kiafya za kulala: Kupunguza fikira nyingi

Ikiwa una shinikizo nyingi, kulala kunaweza kusaidia kupunguza fikira nyingi na kuboresha mfumo wako wa afya. Wataalum wana amini kuwa kulala dakika 30 kunaweza kusaidia.

Kulala mchana kunaweza kusaidia kulala vyema usiku

Hata kama inaonekana kama haiwezekani, kulala mchana kunaweza saidia watu wazima kulala vyema zaidi usiku. Utafiti umeonyesha kuwa kulala dakika 30 katika ya saa saba na saa tisa mchana pamoja na mazoezi ya wastani; kama vile kutembea na kujinyoosha kuna saidia usingizi wa usiku. Afya ya fizikia na kiakili inaweza boreshwa pia.

 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable