42 Wafariki kwenye mafuriko Ujerumani

0

 


Takribani watu 42 wamefariki dunia na wengine kadhaa hawajulikani walipo kufuatia mafurukio makubwa yaliyosababishwa na mvua huko magharibi mwa Ujerumani, Polisi imethibitisha.

Mafuriko hayo yameathiri zaidi majimbo ya Rhineland-Palatinate na Rhine-Westphalia Kaskazini, ambapo majengo kadhaa na magari yamesombwa na maji.

Mafuriko kama hayo yameathiri pia nchi jirani ya Ubelgiji na kusababisha vifo vya watu 6, huku jiji la Liège likiwataka wakazi wake kuhama mara moja.

Mafururiko hayo yanafuatia mvua kubwa kuwahi kunyesha katika eneo la magharibi mwa Ulaya na kusababisha mito mikubwa kupasuka na kumwaga maji kwenye maeneo ya watu.

Nyumba zaidi ya 200,000 hazina umeme huku miundo mbinu kama barabara, reli na mifumo ya maji ikiharibiwa vibaya na mvua hizo zilizonyeshwa kwa zaidi ya saa 24

Mmoja wa viongozi wakubwa wa jimbo la Rhineland-Palatinate Malu Dreyer, ameyaelezea mafuriko hayo kama janga kubwa.

"Kuna vifo, waliopotea na wengine wengi wako kwenye hatari," alisema. "Watoa za dharura wanaendelea na shughuli za uokoaji licha ya kuhatarisha maisha yao."

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, ambaye yuko Marekani kukutana na Rais Joe Biden, amesema ameshitushwa na janga hilo.

Hannah Cloke, profesa kutoka chuo kikuu cha Reading, ameiambia BBC kwamba, kiwango cha vifo vilivyoripotiwa kusababishwa na mafuriko Ulaya kunaonyesha jinsi mifumo iliyopo ilivyoshindwa kufanya kazi.

Baadhi ya mawaziri wa Ujerumani akiwemo waziri wa mazingira, Svenja Schulze aliyeandika katika mtandao wa twitter kwamba: "Mabadiliko ya tabianchi yamewasili Ujerumani", wanaonekana kutoa lawama kwa mabadiliko hayo.

Waziri wa mambo ya ndani Horst Seehofer ameliambia gazeti la Bild kwamba hali ya hewa iliyopo sasa ni athari za wazi za mabadiliko ya tabia nchi, na kutaka nchi hiyo kujiandaa vizuri zaidi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable