Afghanistan:Wanamgambo wa Taliban wameingia katika mji ulio magharibi mwa Afghanistan

0

 

Idadi kubwa ya vikosi vya kigeni vilivyobaki nchini Afghanistan vimeondoka kabla ya tarehe ya mwisho ya tarehe 11 Septemba

CHANZO CHA PICHA,EPA

Wanamgambo wa Taliban wameingia katika mji ulio magharibi mwa Afghanistan wakati wakijaribu kupenya kabla ya vikosi vya Nato kuondoka.

Maafisa wote wa serikali katika mji wa Qala-e-Naw, katika jimbo la Badghis wamehamishiwa kaatika kambi ya karibu ya jeshi, gavana wa eneo hilo ameiambia BBC.

Amesema wanamgambo walikuwa ''wakielekea katikati ya mji'' na kulikuwa na mapambano makali na vikosi vya serikali.

Mafanikio ya Taliban yanakuja wakati Marekani, Uingereza na washirika wanajiondoa baada ya miaka 20.

Local militia have been rallying around Afghan security forces since the withdrawal of Western forces

CHANZO CHA PICHA,REUTERS

Idadi kubwa ya vikosi vya kigeni vilivyobaki nchini Afghanistan vimeondoka kabla ya tarehe ya mwisho ya tarehe 11 Septemba, na kuliacha jeshi la Afghanistan likisimamia usalama.

Vyanzo vya habari vimeiambia BBC kuwa Taliban walihamia gerezani huko Qala-e-Naw na kuwaachilia huru wafungwa 400, wakiwemo zaidi ya wapiganaji 100 wa kundi hilo.

Map

Vikosi vya Afghanistan vinavyolinda gereza hilo vinaripotiwa kujisalimisha bila kupambana.

Gavana Hisamudin Shams alisema alikuwa amewaona Taliban katika wilaya ya Qala-e-Naw anakoishi, na ofisi za makao makuu ya huduma ya ujasusi yamechomwa moto.

Lakini alikanusha ripoti kwamba mji umeangukia kwa Taliban, na akasema wanajeshi wa Afghanistan walikuwa wakiutetea.

Taliban wamekamata wilaya kadhaa katika wiki za hivi karibuni na sasa wanafikiriwa kudhibiti karibu theluthi moja ya nchi. Kufikia sasa miji mikuu ya majimbo imesalia chini ya udhibiti wa serikali.

Chini ya makubaliano na Taliban, Marekani na washirika wake wa Nato walikubaliana kuondoa askari wote kwa ahadi ya wanamgambo kutoruhusu kikundi chochote chenye msimamo mkali kufanya kazi katika maeneo wanayodhibiti.

Lakini Taliban hawakukubali kuacha kupigana na vikosi vya Afghanistan, ambavyo uwezo wao wa kudhibiti waasi unatiliwa shaka.

Rais Ashraf Ghani anasisitiza kuwa vikosi vya usalama vya Afghanistan vina uwezo kamili wa kudhibiti waasi, lakini zaidi ya wanajeshi 1,000 wa Afghanistan walitorokea nchi jirani ya Tajikistan katika siku za hivi karibuni, na pia kumekuwa na ripoti za wanajeshi zaidi wanaotafuta hifadhi Pakistan na Uzbekistan kutoroka vita .

Nchi jirani zinajiandaa kwa utitiri wa wakimbizi ikiwa mapigano yataendelea kuongezeka.

Waziri wa mambo ya nje wa Iran, ambaye nchi yake inashiriki mpaka na Afghanistan, alisema Marekani imeshindwa nchini Afghanistan na uwepo wake umesababisha uharibifu mkubwa kwa nchi hiyo. Mohammad Javad Zarif alikuwa akizungumza huko Tehran wakati wa mkutano kati ya ujumbe wa Afghanistan na wawakilishi wa Taliban.

Mapema wiki, msemaji wa Taliban Suhail Shaheen aliambia BBC kwamba kundi hilo halihusiki na ongezeko la vurugu hivi karibuni. Alisisitiza kwamba wilaya nyingi ziliangukia kwa Taliban kupitia upatanishi baada ya wanajeshi wa Afghanistan kukataa kupigana.

Kwa watu wa Afghanistan, ni wakati wa wasiwasi. Taliban, ambao wameshutumiwa kwa ukiukaji wa haki za binadamu na utamaduni, wanaunga mkono adhabu kama vile kunyongwa hadharani kwa wauaji waliopatikana na hatia - na pia kupiga marufuku televisheni, muziki na sinema, na kutowakubali wasichana zaidi ya miaka 10 kwenda shule.

Vikosi vinavyoongozwa na Marekani viliondoa Taliban kutoka madarakani nchini Afghanistan mnamo 2001. Kikundi hicho kilikuwa kikimhifadhi Osama Bin Laden na wafuasi wengine wa al-Qaeda waliohusishwa na mashambulio ya 9/11 huko Marekani ambayo yalisababisha uvamizi huo.

Taliban waliingia kwenye mazungumzo ya moja kwa moja na Marekani mnamo 2018, na Rais Joe Biden amesema kuwa kujitoa kwa Wamarekani ni haki kwani vikosi vya Marekani vimehakikisha Afghanistan haiwezi kuwa kambi ya wanajihadi wa kigeni kupanga njama dhidi ya Magharibi tena.

Watazamaji wengi wanahoji madai hayo.

Siku ya Jumanne iliripotiwa kuwa jeshi la Marekani liliondoka Uwanja wa Ndege wa Bagram - kituo chake muhimu nchini Afghanistan - usiku bila kuwaarifu Waafghan.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable