Ellen Johnson Sirleaf, rais wa zamani wa Liberia alinusurika mauaji ya 1980 baada ya Serikali ya Tolbert kupinduliwa
Wiki moja iliyopita rais wa zamani wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf aliomboleza kifo cha John G. Bestman ambaye alikuwa mwanasiasa mkongwe nchii humo na waziri wa zamia wa fedha . Bestman alikuwa mtu wa akribu sana na rais wa zamani Sirleaf na hata alikuwa maneja wake wa kampeni alipochagulia kama mwanamke wa kwanza kuwa rais Afrika .
Kifo cha Bestman kilizua kumbukumbu za jinsi alivyosaidia kuleta udhabiti wa kiuchumi nchini humo alipoteuliwa kuwa waziri wa Fedha mwaka wa 1987 baada ya utawala wa Samuel Doe.Mara si moja Sirleaf amekuwa akisimulia historia yake na wanasiasa wakongwe nchini humo na jinsi walivyoepuka kuuawa na utawa wa Doe wakati wa mainduzi ya serikali ya rais William Tolbert.
Katika Makala hii soma kuhusu jinsi Sirlea na wengine walivyonusurika kifo katika mapinduzi yaliyosababisha kuuawa kwa mawaziri kadhaa wa serikali ya Tolbert
Alfajiri moja ya tarehe 22 Aprili mwaka wa 1980 wanaume 13 waliofunikwa nyuso walifikishwa katika fukwe za bahari ya Atlantic.Kilichofuatia kiliwashangaza wengi na hadi leo hapajawahi kutokea ukatili kama huo kwa wanachama wa serikali iliyotolewa madarakani.
Wanaume hao 13 walikuwa nusu uchi ,mawaziri wa zamani wa serikali ya rasi William Tolbert aliyekuwa amepinduliwa siku 10 zilizotangulia .Rais Tolbert mwenyewe akiuawa kinyama na vikosi vya kiongozi aliyechukua madaraka Samuel Doe .
Kilikuwa kitendo ambacho kiliwashangaza wengi duniani na hasa barani Afrika . Mawaziri hao mwanzo walikamatwa katika siku za kwanza baada ya mapinduzi ya tarehe 12 Aprili na mmoja baada ya mwingine wakaanza kufunguliwa mashtaka mbaimbali ikiwemo uhaini.
Samuel Doe alikuwa akiongoza kundi la Waliberia wa asili ya taifa hilo waliokuwa na lalama dhidi ya wazawa wa watumwa kutoka Marekani ambao walikuwa wanaitawala Liberia tangu nchi hiyo ianzishwe miaka kadhaa hapo nyuma .
Doe wakati huo akiwa na umri wa miaka 29 pekee alikuwa akiliongoza kundi la Armed Forces of Liberia (AFL) ambalo lilikuwa limechukua madaraka na kuongoza serikali ya mpito hadi alipuuawa Septemba mwaka wa 1990 wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe .
Kutembezwa uchi barabarani
Baada ya mapinduzi kulikuwa na hofu kote nchini Liberia huku watu kadhaa wakikakamatwa na wengine kuuawa na vikosi vya serikali mpya .Miongoni mwa waliokamatwa ktika misako ya akati huo ni mawaziri 13 waliokuwa wa serikali ya rais Tolbert ambao mauaji yao hadharani na yaliyopeperushwa mubashara katika runinga ya taifa yaliwatamaushwa wengi nje na ndani ya Liberia .
Mawaziri hao walitembezwa wakiwa uchi katika barabara za Monrovia wakionyeshwa kwa umma kisha wakafungwa kwenye miti iliyokuwa imesimamishwa katika ufuo wa bahari ya Atlantic.
Watu wengi hawakuamini kilichokuwa kikifanyika na hata palikuwa na matumaini kamba mauaji hayo ya hadharani na kikatili hayangefanyika kwasaabu nchi mbali mbali zilikuwa zimelaani vikali ukosefu wa usalama nchini Liberia baada ya serikali mpya kuchukua madaraka .
Muda mfupi baada ya kufikishwa katika ufuo wa bahari ambako nyuo zao zilifungwa kwa vitambaa ,kikosi kilichokuwa kimejihami kwa bunduki kiliwafyatulia risasi mawaziri hao mmoja baada ya mwingine na kuwaua wote . Wote walinyimwa kabisa haki ya kuwakilishwa na wakili au kujitetea na hapo ndipo Liberia ilipojipata katika hali ya hofu .
Watu hao waliokufa ni pamoja na mawaziri kadhaa wa zamani wa baraza la mawaziri na kaka mkubwa wa William Tolbert, rais aliyeuawa wa nchi hiyo .
Waandishi wa habari ambao walikuwa wamepelekwa kwenye kambi ili kutazama mauaji hayo walisema yalijaa ukatili .
Walisema wanaume wanne walilazimishwa kutazama wengine wakifa kabla ya kupigwa risasi kwani kulikuwa na vigingi tisa tu.
Wanaume hao 13 walikuwa wameshtakiwa kwa uhaini, ufisadi na ukiukaji wa haki za binadamu.
Walakini, ni wanne tu waliohukumiwa kifo baada ya kusikilizwa kwa kesi yao na mahakama ya kijeshi.
Lakini hukumu za mahakama hiyo zilifutwa na ile inayoitwa "Baraza la Ukombozi", iliyoongozwa na Sajenti Samuel Doe.
Ni mawaziri wanne tu wa utawala wa Tolbert walionusurika mapinduzi na matokeo yake; miongoni mwao alikuwa Waziri wa Fedha na Rais wa baadaye Ellen Johnson Sirleaf ,Makamu wa Rais Bennie Dee Warner na waziri wa Kilimo Florence Chenoweth.
Chenoweth aliweza kutorokea nchi jirani ya Sierra Leone kabla ya kwenda Marekani wakati Warner alikuwa nje ya nchi wakati wa mapinduzi.
Warner alijaribu bila mafanikio kuanzisha serikali iliyokuwa uhamishoni kabla ya Doe kumpa msamaha na ruhusa ya kurudi Liberia mnamo 1984.
Awali Sirleaf alikuwa kizuizini lakini baadaye akapewa nafasi katika serikali ya Doe ambayo awali alikubali, lakini baadaye aliikimbia nchi hiyo kwenda Marekani baada ya kukosoa hadharani sera za Doe. Sirleaf na Chenoweth baadaye walirudi kwenye siasa za Liberia baada ya kifo cha Doe.
Orodha ya waliouawa siku hiyo
• Frank E. Tolbert — Kakake rais Tolbert na rais wa bunge la seneti
• Richard A. Henries — spika wa bunge la wawakilishi
• E. Reginald Townsend — mwenyekiti wa kitaifa wa chama cha True Whig
• P. Clarence Parker II — Mwenyekiti wa baraza la uwekezaji nan a mweka hazina wa chama cha True Whig
• James A. A. Pierre — Jaji mkuu wa mahakama ya juu Zaidi
• Joseph J. Chesson Sr— Waziri wa Haki
• Cecil Dennis — Waziri wa masuala ya Kigeni
• Cyril Bright — waziri wa zamani wa Uchumi na Mipango
• John W. Sherman — waziri msaidizi wa biashara
• James T. Phillips — waziri wa zamani wa Fedha
• David Franklin Neal — waziri wa zamani wa mipango na Uchumi
• Charles T. O. King — Naibu waziri wa Kilimo
• Frank J. Stewart Sr. — Mkurugenzi wa Bajeti
Utawala wa Samuel Doe
Kufuatia mapinduzi hayo, Doe alichukua cheo cha Jenerali na akaanzisha Baraza la Ukombozi wa Watu (PRC), lililojumuisha yeye mwenyewe na maafisa wengine 14 wa vyeo vya chini, kutawala nchi.
PRC ilivunjwa baada ya uchaguzi mkuu wa 1985, ambapo Doe alichaguliwa kuwa rais; aliapishwa mnamo 6 Februari 1986. Ingawa Doe alijionyesha kama mkombozi na mtu ambaye ataleta afueni na demokrasia zaidi nchini, utawala wake ulituhumiwa kwa ubabe na kwa kuwabagua vikali watu wa makabila mengine.
Doe aliendelea kutawala nchi hadi alipouawa mnamo 9 Septemba 1990 na INPFC, ikiongozwa na Prince Johnson, wakati wa Vita vya kwanza vya wenyewe kwa wenyewe
Mnamo Agosti 2008, mbele ya Tume ya Ukweli na Maridhiano (TRC) huko Monrovia, waziri wa zamani wa sheria wa Doe, Chea Cheapoo - ambaye alishiriki uchaguzi wa Rais wa Liberia wa 2011 - alidai CIA ilitoa ramani ya Jumba la Rais , kuwezesha waasi kuingia ndani ; na kwamba ni afisa mzungu wa shirika la CIA aliyempiga risasi na kumuua Tolbert; na kwamba Wamarekani "walihusika na machafuko yaliyofuatia baadaye nchini Liberia".
Mauaji ya Samuel Doe
Waasi wakiongozwa na Charles Taylor na Prince Johnson walikuwa wameanzisha harakati za kumuondoa Doe madarakani na kwa miezi mitatu alikuwa amejifungia katika jumba lake la Monrovia akiwa amezingirwa na walinzi waliojihami vikali. Kuna uvumi kuhusu jinsi Doe alivyosalitiwa na mmoja wa washirika wake wa karibu kutoka nje kabla ya waasi kumpata na kumkamata .
Mwandishi wa BBC aliyekuwa katika makao makuu ya kikosi cha walinda amani cha Afrika Magharibi alishuhudia tukio hilo zima hadi rais Doe alipochukuliwa na waasi huku miili ya walinzi wake ikiachwa imetapakaa kote katika ofisi za makao hayo .
Prince Johnson alisema rais Doe angeshtakiwa na kuhukumiwa lakini ulimwengu haukujua kwamba hukumu yake ingekuwa kifo na ingejiri siku hiyo hiyo . Picha za video zilimuonyesha rais akipiga magoti akimlilia Prince Johnson kumsamehe na yamkini ombi lake hilo la huruma halikumshtua Johnson .
Milio ya risasi iliripotiwa kuzuka muda mfupi baada ya Doe kuondoka katika jumba lake la kifalme kwa ziara isiyopangwa kwa makao makuu ya Mghana Jenerali Arnold Quainoo, kamanda wa jeshi la Afrika Magharibi, kulingana na BBC.
Johnson na baadhi ya vikosi vyake walimfuata Doe, na ugomvi ukaibuka ambao ukawa ufyatulianaji wa risasi wa muda mrefu , uliohusisha kurushwa kwa magruneti , ripoti ya BBC ilisema. Wanajeshi wa Johnson walimjeruhi Doe na kumpeleka kwenye kambi yao, iliongeza.
Tukio la siku hiyo lilikuja siku chache tu baada ya Doe na Johnson kuripotiwa kukubaliana rasmi kusitisha mapigano, ambayo yalisababisha vifo vya watu 5,000 na kuwaacha zaidi ya watu 500,000 wakiwa hawana makazi. Doe na Johnson wote wawili walikuwa wamekaribisha juhudi za kulinda amani za Afrika Magharibi.


