Mchoro wa kumkumbuka Jacob Maseko nyumbani kwao Spring
Job Maseko, raia wa Afrika Kusini na shujaa wa Vita Vikuu Vya Pili vya Dunia, alinyimwa medali ya juu zaidi ya kijeshi kwa sababu alikuwa mweusi.
Hiyo ndio sababu kundi la wanaharakati linapinga kile kilichosukuma familia yake kuanzisha mpango wa kutaka juhudi zake kutambuliwa baada ya kufa.
Licha ya kuchukuliwa kuwa shujaa wa vita, Maseko alifariki akiwa masikini mwaka 1952.
Kukanyagwa vibaya na gari moshi akiwa na umri wa miaka 36, na juhudi za ushujaa wake uko katika hatari ya kusaulika.
Miaka 10 kabla ya hapo, alipokuwa mfungwa wa vita, alitumia kilipuzi cha kujitengenezea kulipua shehena ya Wajerumani kwenye nanga huko Tobruk Libya.
Aliporejea Afrika Kusini, hakupewa heshima iliyopewa mashuja kizungu walioshirika katika vita, hali inayoangazia sera za kibaguzi zilizokuwepo wakati huo. Baadhi ya watu wanaamini kwamba ubaguzi ulidhihirika na jinsi thamani yake ilivyotambuliwa.
Alipokea medali ya kijeshi "kama hatua nzuri ya kijasira", lakini mwanaharakati Bill Gillespie anaamini hakupewa tuzo ya Victoria Cross ambayo ni heshima ya juu, kwa sababu alikuwa mweusi na ameanzisha kampeni ya kushinikiza apewe tuzo hiyo.
Mpwa wa Maseko anaamini kuwa ubaguzi ndio sababu uliofanya asipewe tuzo ya heshima
"Machungu na ufahari"
Familia ya Maseko inaunga mkono mpango huo.
"Najivunia mchango wake, lakini pia namhurumia. Tunaamini laiti angelikuwa mzungu angelikuwa amepewa heshima kubwa sana," anasema mpwa wake Jennifer Nkosi Maaba aliiambia BBC, akiweka shada la maua kwenye kaburi lake.
Maafisa 80,000 weusi kutoka Afrika Kusini walihudumu katika jeshi la kitaifa (NMC). Baada ya vita walipewa baisikeli, viatu, na baadhi yao kupewa suti, kama zawadi. Maafisa wazungu walipewa zawadi ya nyumba na ardhi.
Mamlaka za Afrika Kusini hawaakuwa tayari kuangazia na kusifia mchango wa Maseko "kwani iliashiria uwezeshwaji kupitia huduma ya jeshi ambayo serikali ilitaka kuzima," anasema mwanahistoria Suryakanthie Chetty.
Wnachama wa NMC hawakupewa bunduki, lakini walibeba silaha za kitamaduni na ambazo hazikuchukuliwa kama silaha kwani zilikuwa zikitumiwa na wafanyakazi, mabawabu na maafisa wa afya.
Maseko aliwahi kuhudumu kama machela kwa vikosi vya ushirika Afrika Kaskazini, ambako zaidi ya mara moja aliwaokoa wanaume waliojeruhiwa wakikabiliana na maadui.
Lakini mnamo Juni 1942 alipelekwa jela wakati kamanda wake alipojisalimisha kwa Wajerumani katika eneo la Tobruk. Huko alilazimishwa kupakua mizigo kutoka kwa meli bandarini.
Kwa kutumia ujuzi aliopata kwa kufanya kazi katika migodi ya dhahabu nchini Afrika Kusini, Julai 21 Maseko alichanganya unga wa risasi na mafuta ya gari na kuweka kwenye dramu sehemu ya chini ya meli ambayo ilizama baada ya mlipuko, kulingana na maelezo rasmi yaliyoambatanishwa na medali ya kijeshi.
"Alionesha ujasiri na kutokuwa na wasiwasi kabisa juu ya uwezekano wa kuadhibiwa na adui au kujeruhiwa katika mlipuko aliotengeneza mwenyewe."
"Anastahili zawadi kubwa zaidi kuliko viatu na baisikeli kwa ushujaa wake ... anastahili kupewa tuzo ya Msalaba wa Victoria kwa sababu ujasiri wake lifunza dunia uweledi wa jeshi la Afrika kusini," alisema Nkosi Maaba alipoulizwa kuhusu hatua iliyochukuliwa na mjomba wake miaka 80 iliyopita.
Gillespie anaamini kuwa rangi ya ngozi yake ilisababisha mamlaka kumpigia kura ya turufu kupinga asipewe tuzo ya mapambo ya juu zaidi.
"Nina hakika kabisa. Nishani ya Kijeshi waliyompa ilikuwa tu zawadi ya faraja, "anasema mwanaharakati huyo, mtoto wa mpiganaji mwingine wa Afrika Kusini katika Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.
Miezi kadhaa baada ya kifo chake, sherhe ya kidini ilifanywa kwa hwshima ya Maseko.
Alan Sinclair, msimamizi wa Jumba la kumbukumbu la Kitaifa la Historia ya Kijeshi, ambalo makao makuu yake yana picha ya Maseko, pia anaamini anapaswa kupokea tuzo ya ya hali ya juu.
"Cha kusikitisha ni kwamba Waafrika Kusini weusi waliojitolea kijeshi kama wenzao wazungu walidhulumiwa. Binafsi nahisi, Maseko alistahili kupewa tuzo ya juu ya mashujaa," Sinclair aliiambia BBC.
Lakini kulingana na Keith Lumley, ambaye anaongoza Wakfu wa Victoria Cross Foundation, ambayo intunza kumbukumbu ya wale walopwe tuzo hiyo ya juu, huenda kulikuwa na sababu nyingine kwa nini Maseko hakutunukiwa.
"Bila shaka kazi aliyofanya ya kulemaza meli ilikuwa hatari sana na huenda angeliuawa laiti angelijulikana," anasema Lumley.
"Walakini, haonekani kufikia kiwango cha Msalaba wa Victoria, kwa sababu hakuna mtu aliyemshuhudia. Ingawa hakuna shaka kwamba alifanya kile alichofanya ... hakuna mtu aliyemwona akifanya hivyo. Tumesoma kuwa medali ya kijeshi ilikuwa ishara ya matendo yake ".
Hata Wizara ya Ulinzi ya Uingereza, ambayo ilishirikiana na Afrika Kusini wakati wa vita Vikuu Vya Pili vya Dunia, haikuna haja ya kuangalia upya tuzo ya shujaa Maseko.
Tunapothamini mchango wa Waafrika Kusini walishiriki katika vifa hivyo, "hatuwezi kuangazia tuzo hizo kwasababu hatuna uwezo wa kuthibitisha mazingira na kulinganisha mchago wao katika tukio lililofanyika miaka mingi iliyopita ,"msemaji alielezea BBC kupitia barua pepe.
Sanamu ya ya kumuenzi Job
Juhudi za Gillespie kushinikiza wizara kubadili sera hizo ziligonga mwamba wakati bunge la Uingereza lilipopinga utafiti wa suala hilo lenye utata.
Ilkataliwa kwa sababu mkakati kama huu hauwezi kuomba mtu atunukiwe.
Gillespie anaafiki kuwa mchango wa Maseko unastahili kukumbukwa zaidi.
"Kumekuwa na visa vya kuharibiwa kwa sanamu za wakoloni, laikini mwaonaje tukiweka moja ya Job Maseko? Bila shaka hatua hiyo itakuwa kumbukumbu yake ya daima."
Katika mji alikozaliwa, wengi bado wanamkumbuka Job Maseko.
Lumley inatoa matumaini, akibainisha kuwa Teddy Sheean wa jeshi la wanamaji la Australia alipewa Msalaba wa Victoria mnamo Novemba mwaka jana kwa kitendo kilichofanyika mnamo 1942 baada ya miaka 50 ya ushawishi wa familia yake.
"Kuhusu suala Job, siwezi kusema kwanini hakupewa tuzo ya Msalaba wa Victoria , lakini kazi zaidi inahitajika kupata maelezo hayo ya ziada ambayo yangefanya tuzo yake ifae
Lakini katika eneo la Kwa-Thema, jamii ya Kiafrika katika kijiji chaa Springs alikozaliwa, Maseko bado anaenziwa , kuna barabara na shule ya msingi iliyopewa jina lake pamoja na ukuta mkubwa uliyo na picha yake.
Kando ya kaburi, mpwa wake alielezea kufarijika kwake na kufufuliwa kwa juhudi za kumuenzi.
Akiangalia kaburi lake, Bi. Nkosi anasema kwa kujigamba, "Daima tutakukumbuka, mjomba. Endelea kupumzika kwa amani."
Nomsa Maseko ni jamaa wa mbali wa Job, lakini hajahusika katika kampeni iliyozinduliwa na jamaa wake wa karibu.



