Picha iliyochukuliwa kutoka juu na droni inayoonesha makaburi baada ya mafuriko yaliyotokea katika eneo la Bad Neuenahr-Ahrweiler, Ujerumani.
Mafuriko mabaya zaidi kuwahi kushuhudiwa kwa miongo
Hiyo ndio hali ambayo Ujerumani na Ubelgiji zimeishuhudia wiki hii, ambako watu zaidi ya 150 wameripotiwa kufa.
Mvua imesababisha maji ya mito kufurika na kumwagika nje ya kingo zake, uharibifu mkubwa katika eneo hilo na baadhi ya vijiji vimeangamizwa kabisa.
Wataalamu wanasema kwamba janga la mafuriko barani Ulaya ni sehemu ya historia ya majanga yaliyotangazwa na kwamba yanatokana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Wataalamu wengine wanasema japokuwa dalili mbaya za hali ya hewa zilitangazwa kuhusu mvua inayokuja, hazikutarajiwa kuwa na athari za kiwango kikubwa cha aina hiyo. Wanasema vifaa bora zaidi vya utabiri wa hali ya hewa vinahitajika.
" Ukamuaji wa maji zaidi"
Sababu nyingi zinachangia kutokea kwa mafuriko, lakini hali ya hewa ya joto inayosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa inaongeza uwezekano wa kunyesha kwa mvua kubwa.
Tayari dunia imechemka kwa kiwango cha nyuzi joto 1.2 , tangu ilipoanza enzi ya viwanda na viwango vya joto vitaendelea kupanda hadi serikali za dunia zitakapo punguza utoaji wa hewa chafu ya kaboni kwa kiwango cha CO2.
"Matukio ya hali ya hewa kama haya yanayoshuhudiwa (katika bara la Ulaya ) hutokea mara kwa mara. Lakini sasa, kutokana na kuongezeka kwa ujumla kwa hali ya hewa ya joto na kupanga kwa viwango vya joto, hewa inaweza inaweza kuwa na maji zaidi ya mvuke ," alisema Thomas Endrulat kutoka taasisi ya huduma za hali ya hewa ya Ujerumani , katika mahojiano na Shirika la habari la Reuters.
"Kwa hiyo mkusanyiko huu unapotokea, maji zaidi yanakamuliwa nje ya wimbi kwasababu ya mabadiliko ya hali ya hewa," aliongeza.
Nyumba zilizoangamia katika eneo la Pepinster, Ubelgiji
Akizungumzia hususan utabiri wa hali ya hewa uliotolewa kwa Ujerumani kabla ya mafuriko haya , mtaalamu huyo alisema kwamba tahadhari zilitolewa kwa muda unaofaa, lakini kulikuwa na mambo mengine ambayo hayawezi kutabirika.
"Tahadhari zilitolewa kwa muda uliofaa. Lakini kile kilichotokea ni kigumu zaidi na kinategemea historia na myeyuko wa udongo, hali ya mabwawa na hifadhi za maji .Na pia inategemea na muda tukio hilo linapotokea : Kama kitu kama hiki kitatokea usiku, kama watu hawajui dalili zina maana gani, au ni vigumu kuwafikia kwa njia ya vyombo vya habari , "Endrulat anaeleza.
"Hali hizo hutofautiana kila mara. Na ndio maana ni vigumu zaidi kuliko utabiri wa kawaida wa hali ya hewa," anatatmini.
Unaweza pia kusoma:
Kwa upande wake, Waziri wa mazingira wa North Rhine-Westphalia, Ursula Heinen-Esser, nchini Ujerumani alisema Ijumaa kuwa sababu kuu ya maafa ya mafurika ni mabadiliko ya hali ya hewa.
"Changamoto ni kwamba wakati mwingine tunalazimika kukabiliana na ukame wa kupindukia na wakati mwingine mvua ya kupindukia," aliliambia gaziti la eneo hilo la Koelner Stadt-Anzeiger.
Udongo "unaweza kushindwa kunyonya maji zaidi kutokana na ukame uliotolea miaka iliyopita na mvua katika wiki za hivi karibuni," alisema, akiongeza kuwa hiyo ndio hali iliyopo sasa "Haiwezekani kuishugulikia kwa kipindi kifupi ."
Janga la kihistoria lililotangazwa
Wanasayansi wamekuwa wakitabiri kwa miaka mingi kwamba mvua na mawimbi ya joto yatakuwa makubwa zaidi kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Na wamekuwa wakiwaonya mara kwa mara wanasiasa kwamba kuna haja ya kuwalinda raia dhidi ya majanga yanayosababishwa na hali ya hewa, kama vile mafuriko yaliyotokea Ulaya na joto kubwa ambalo liliikumba Marekani miaka michache iliyopita.


