MTIBWA SUGAR YABAKIZA DK 180 ZA MOTO

0

 


KIKOSI cha Mtibwa Sugar kinachonolewa na Kocha Mkuu, Badru Mohamed kimebakiza dk 180 za moto kukamilisha mzunguko wa pili ndani ya Ligi Kuu Bara.

Mechi hizo mbili ni za maamuzi ya timu hiyo kubaki kwa kuwa ikiyeyusha pointi sita haitakuwa na uhakika wa kubaki ndani ya ligi msimu ujao wa 2021/22.

Kikiwa kimecheza jumla ya mechi 32 kimekusanya pointi 38 kipo nafasi ya 11 kwenye msimamo na vinara ni Simba wenye pointi 76 baada ya kucheza mechi 31.

Mechi zake mbili ambazo ni dk 180 ni dhidi ya  Dodoma Jiji iliyo nafasi ya 9 na pointi 42 itapigwa Julai 14, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Kigongo chake cha mwisho ni dhidi ya JKT Tanzania iliyo nafasi ya 14 na pointi 36 itakuwa Julai 18, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.  

Pointi hizo zinaweza kufikiwa na Mbeya City iliyo nafasi ya 13 na pointi 36 baada ya kucheza jumla ya mechi 32.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable