Namna 'masaji' ya mwili kutumia kisu inavyopendwa Taiwan

0

 

Kukandwa kwa kutumia kisu kulianzia China zaidi ya miaka 2000 iliyopita

CHANZO CHA PICHA,LOUISE WATT

Nikiwa nimelala uso ukiwa umeegemea meza maalumu ya kukanda, nilisubiri kwa hofu. Mtaalamu wa kuchua kwa kutumia kisu, Elsa, kwa bashasha alikuwa ameshika visu viwili. Hii ni kwasababu wakati mwendo wa kukata unatarajiwa katika kuukanda mwili, katika hii, visu hufanya mithili ya ukataji.

Elsa alianza kwa kutumia mikono yake kuukanda mwili wangu. Kisha visu baridi, vya chuma vilianza kupita, juu ya mgongo wangu, mikono na kichwa changu. Nisingejua kuwa visu vilikuwa kazini kama haikuwa sauti ya visu vilivyokuwa vinagongana mara kwa mara.

Wakati kukata kulimalizika, lazima ningekuwa nimelala. cha kushangaza, watu wengi husinzia wanakandwa na visu kwa dakika 70.

Ingawa inaonekana kuwa hatari, daoliao, ambayo hutafsiriwa kama "masaji ya kisu" au "tiba ya kisu", inaaminika kuwa na nguvu za uponyaji wa mwili na kihemko na ni aina ya dawa ya Wachina ambayo inadhaniwa kuwa na zaidi ya miaka 2,000. Wataalamu wanasema ilifanywa kwanza na watawa katika China ya zamani. Ilienea hadi Japan katika Enzi ya Tang zaidi ya miaka 1,000 iliyopita na kwa Taiwan kufuatia Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya China miaka ya 1940.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable