Saba washikiliwa tukio la bweni, maabara kuteketea kwa moto

0

 






Geita. Watu saba wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Geita wakihusishwa na tukio la moto ulioteketeza chumba cha darasa na maabara mbili za sayansi katika Shule ya Sekondari Geita.

Wanaoshikiliwa kwa mahojiano ni walinzi wanne pamoja na wanafunzi watatu wa shule hiyo.

Matukio ya moto katika shule hiyo yalitokea kwa siku mbili mfululizo ambapo tukio la kwanza lilitokea Julai 5,2021 saa 2 usiku na kuteketeza magodoro na masanduku ya vifaa vya wanafunzi  vilivyokuwa vimehifadhiwa kwenye moja ya chumba cha darasa.

Tukio jingine limetokea Julai 6, 2021 saa 4 usiku ambapo moto ambao chanzo chake hakijajulikana uliteketeza vyumba viwili vya maabara za sayansi na kusababisha vifaa vilivyokuwa ndani ya maabara pamoja na majengo  kuteketea.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada wa magodoro, masanduku, madaftari na mashuka kwa wanafunzi zaidi ya 240 walioathirika na tukio hilo ili waweze kuendelea na masomo mkuu wa mkoa huo, Rosemary Senyamule aliwataka wanafunzi kutokuwa na hofu kwa kuwa ulinzi umeimarishwa.

Amesema vifaa hivyo vilivyotolewa na Serikali kwa vina thamani ya Sh35 milioni na kwamba changamoto kubwa kwa sasa ni namna ya kurudisha miundo mbinu iliyoharibiwa.

Amesema majengo yaliyoathirika na moto yameharibika vibaya na hayafai kukarabati na kuwaomba wadau kujitokeza kusaidia vifaa kama mabati, saruji na vifaa vingine vya ujenzi ili yaweze kujengwa upya.

Katika hatua nyingine  amewataka wazazi wa wanafunzi waliochaguliwa kuingia kidato cha tano kutokuwa na hofu na kuendelea kubaki na watoto nyumbani na badala yake amewataka wawaruhusu wanafunzi kuripoti shule  kwa kuwa hadi sasa takwimu zinaonyesha waliopangiwa shule hiyo wengi hawajaripoti.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable