Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 08.07.2021: Ramos, Haaland, Guardiola, Richarlison, Jorginho, Ramos, Goretzka

0

 

Sergio Ramos

CHANZO CHA PICHA,PSG/TWITTER

Paris St-Germain imemsajili Sergio Ramos kwa kandarasi ya miaka miwili baada ya mchezaji huyo kuondoka katika klabu yake ya miaka mingi Real Madrid.

Ramos , 35 aliondoka Madrid baada ya miaka 16 wakati kandarasi yake ilipokamilika mwisho wa mwezi Juni.

Mchezaji huyo ambaye ameichezea mara nyingi zaidi timu yake ya taifa kushinda mchezaji yeyote yule ,ameshinda mataji matano ya La liga na mataji manne ya kombe la klabu bingwa akiichezea Real Madrid.

Ruka Twitter ujumbe, 1

Mwisho wa Twitter ujumbe, 1

Mwenyekiti wa PSG Nasser al khelafi alisema: 'Paris inamkaribisha mchezaji maarufu wa enzi yetu''.

Chelsea wanajiandaa kutoa kitita cha £150m kwa ajili ya mshambuliaji wa Borussia Erling Braut Haaland na tayari klabu hiyo ya Stamford imeshafanya mazungumzo na upande wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Norway. (90 Min)

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola anasema klabu hiyo "haiwezi kumudu gharama" za mshambuliaji mpya na "kuna kila dalili" mabingwa hao wa ligi kuu England wasisajili mshambuliaji msimu huu. (TVS, via Mail)

Haaland

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Haaland

Meneja wa Real Madrid Carlo Ancelotti ameiambia klabu hiyo angetamani kumsajili mshambuliaji wa Kibrazil Richarlison, 24, kutoka klabu yale ya zamani ya Everton. Klabu hiyo ya La Liga inaangalia kama hilo linawezekana. (ESPN)

Wakala wa kiungo wa Chelsea Jorginho, 29, anasema zipo timu zinazomuhitaji mchezaji huyo wa kimataifa wa Italia lakini anatarajiwa kuongeza mkataba mpya wa kusalia 'the Blues' zaidi ya mwaka 2023. (Radio Marte, via Metro)

Nahodha wa RB Leipzig Marcel Sabitzer, 27, anaweza kupatikana kwa ada ya £17m, wakati huu kiungo huyo wa Austria akiingia miezi yake 12 ya mwisho ya mkataba wake na mazungumzo kuhusu mkataba mpya yakiwa bado yanasuasua. (90 Min)

Jorginho

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Jorginho

Wolves imekubali kumuuza beki wake wa kireno, Ruben Vinagre, 22, kwenda Sporting Lisbon kwa ada ya £8.6m. (Football Insider)

Tottenham wanamfuatilia beki wa Sassuolo Mert Muldur, huku West Ham wakitajwa kumtaka pia nyota huyo wa kimataifa wa Uturuki mwenye umri wa miaka 22. (Mail)

Meneja wa Bayern Munich Julian Nagelsmann amesema kiungo wa Ujerumani Leon Goretzka, anayehusishwa kutakiwa Manchester United, ni mchezaji "muhimu" wa klabu hiyo na "atafurahi kufanya naye kazi kwa miaka mingi ijayo". (Goal)

Leon Goretzka

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Leon Goretzka

AC Milan itaongeza dau lake kwa ajili ya kiungo wa Ivory Coast Franck Kessie wakijaribu kuongeza mkataba wa nyota huyo mwenye umri wa miaka 24. (Gazzetta dello Sport)

Kiungo wa Italia Davide Calabria, 24, amekubali kusaini mkataba mpya, utakaombakiza AC Milan mpaka 2025. (Calciomercato, via Football Italia)

Southampton wana uhakika wa kunasa saini ya mshambuliaji wa Kiingereza Adam Armstrong, 24, kutoka Blackburn Rovers kwa ada ya £10m. (Football League World)

Middlesbrough iko katika mazungumzo mazuri ya kumsajili kiungo wa Atletico Banfield Martin Payero, ambaye yumo kwenye kikosi cha Argentina kitakachoshiri michezo ya Olympic huko Tokyo msimu huu. (Football Insider)

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable