Tetesi za soka Ulaya Jumamosi tarehe 17.07.2021: Kane, Grealish, Ronaldo, Bale, White, Trippier, Zaha, Locatelli

0

 

Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane

Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane, 27, na mshambuliaji wa Aston Villa Jack Grealish, 25, wamesalia kuwa wachezaji wanaolengwa zaidi na Manchester City msimu huu na washindi hao wa Primia Ligi wameazimia kusaini mkataba na wachezaji hao wa kimataifa wa England . (Athletic - subscription required)

Mchezaji nyota wa Villa Grealish, hatahivyo badao anatarajiwa kusaini mkataba mpya na na klabu ya West Midlands. (Birmingham Mail)

Mshambuliaji wa Wales Gareth Bale
Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa Wales Gareth Bale

Real Madrid wamelazimika kuachana na mshambuliaji wa Wales Gareth Bale kwa ajili ya msimu mwingine kwasababu hawajapokea ofa zozote kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 ambaye amekuwa Tottenham kwa mkataba wa deni. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Arsenal wamefikia mapatano ya kimsingi na Brighton juu ya mkataba na mlinzi wa England Ben White, 23, wenye thamani ya takriban pauni milioni 50. (Athletic - subscription required)

Mshambuliaji wa Ivory Coast Wilfried Zaha

CHANZO CHA PICHA,REUTERS

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa Ivory Coast Wilfried Zaha

Crystal Palace wanatumai juhudi zilizofanyika katika kuimarisha kikosi chini ya meneja mpya Patrick Vieira zitatosha kumshawishi mshambuliaji wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 28, kubakia katika klabu hiyo. (Standard)

Inter Milan wameanza juhudi za kusaini mkataba na mlinzi Mhispania Hector Bellerin kutoka Arsenal, lakini machampioni hao wa Italia wanamtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kwa mkataba wa mkopo wa mwaka mmoja wakiwa na chaguo la kuufanya kuwa wa kudumu msimu ujao , huku the Gunnerswakitaka takriban pauni milioni 15. (Sun)

Mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo, 36
Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo, 36

Mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo, 36

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo, 36

Mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo, 36, ambaye amekuwa akihusishwa na taarifa za kurejea Manchester United na kuhamia Paris St-Germain, yuko tayari kuendelea kubakia katika Juventus msimu ujao huku kukiwa na mazungumzo ya uwezekano wa kusaini mkataba wa mwaka mmoja yanayoweza kujumuisha kukatwa kwa malipo yake. (Gazzetta dello Sport - in Italian)

Meneja wa Tottenham Nuno Espirito Santo anaweza kurejea katika klabu yake ya zamani Wolves katika juhudi za kuwaajiri wachezaji msimu huu, huku mlinzi wa Ivory Coast Willy Boly, 30, na mshambuliaji wa Ureno, 25, Daniel Podence akihusishwa na taarifa za kuhamia katika klabu hiyo iliyopo kaskazini mwa London. (talkSport)

Kiungo wa kati wa Norway Martin Odegaard

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Kiungo wa kati wa Norway Martin Odegaard

Arsenal bado wanamtaka kiungo wa kati wa Norway Martin Odegaard, 22, baada ya mkataba wake kumalizika msimu uliopita na meneja wa Gunners Mikel Arteta yuko tayari kama kumchukua kama Real Madrid wako tayari kumuachilia aende tena. (Athletic - subscription required)

Burnley wamewapiku machampioni wa Ulaya Chelsea katika mbio za kusani mkataba na mlinda lango, raia wa Wales mwenye umri wa miaka 35 Wayne Hennessey baada ya kuondoka katika Crystal Palace . (Football Insider)

Harry Wilson, mchezaji anayetaka kuuzwa

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Hai ya baadaye ya Harry Wilson katika Arsenal iko mashakani

Harry Wilson ni miongoni mwa wachezaji 10 ambao Liverpool inataka kuwauza na itakubali malipo ya pauni milioni 10 kwa ajili ya mshambuliaji huyo wa Wales 24, ambaye amekuwa akihusishwa na klabu za Brentford, West Brom na Benfica. (Mirror)

Mchezaji wa kimataifa wa Italia Manuel Locatelli
Maelezo ya picha,

Mchezaji wa kimataifa wa Italia Manuel Locatelli

Sassuolo wamemuweka kiungo wa kati wa Serbia anayecheza katika Liverpool Marko Grujic, 25, kama mchezaji anayeweza kukaba nafasi ya mchezaji wa kimataifa wa Italia Manuel Locatelli, 23, ambaye amehusishwa na taarifa za kuhamia who Arsenal a na Juventus, msimu huu. (Sky Sports)

Kiungo wa kati wa Atletico Madri 26, Mhispania Saul Niguez, ambaye amekuwa akihusishwa na Barcelona kama sehemu ya mpango wa kubadilishana wachezaji kwa ajili ya Antoine Griezmann, 30-anasakwa na klabu za Liverpool na Manchester United pia. (AS - in Spanish)

Atletico wamesalia kuwa mstari wa mbele katika kusaini mkataba na Griezmann

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Atletico wamesalia kuwa mstari wa mbele katika kusaini mkataba na Griezmann

Atletico wamesalia kuwa mstari wa mbele katika kusaini mkataba na Griezmann, lakini Chelsea, Manchester City na Liverpool wamefahamishwa kuwa mshambuliaji huyo Mfaransa anaweza kupatikana kwa "gharama ndogo". Walau timu mbili za Primia Ligi zimezungumza na wakala wake miezi iliyopita. (90min)

kiungo wa kati wa timu ya Ufaransa ya Lyon , Houssem Aouar
Maelezo ya picha,

Kiungo wa kati wa timu ya Ufaransa ya Lyon , Houssem Aouar

Liverpool wanaweza kushawishika kumnunua kiungo wa kati wa timu ya Ufaransa ya Lyon , Houssem Aouar, 23,ambaye amekuwa akihusishwa na Tottenham, Arsenal na Manchester United. (ESPN)

Valencia ni miongoni mwa klabu kadhaa za Uhispani zinazomtaka mshambuliaji wa klabu ya Uingereza- Leeds United Helder Costa, mwenye umri wa miaka 27. (Athletic - subscription required)

Mlinzi wa England Kieran Trippier, 30

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Mlinzi wa England Kieran Trippier, 30

Mlinzi wa England Kieran Trippier, 30 ana matumaini ju ya kujiunga na Manchester United kutoka Atletico Madrid msimu huu na alifanya mipango ya kuhama kabla ya kuanza kwa michuano ya Euro 2020. (Manchester Evening News)

Kiungo wa kati wa AZ Alkmaar Mholanzi Koopmeiners amezivutia timu tatu ikiwemo timu ya Jose Mourinho Roma, klabu ya Ufaransa Rennes pamoja na Arsenal, ambaye anaonekana kama mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kama anayeweza kukaba nafasi ya Mswizi anayehusishwa na Roma- Granit Xhaka, 28. (De Telegraaf - via Team Talk)

Mshambuliaji wa klabu ya Uingereza Northampton Town Caleb Chukwuemeka

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa klabu ya Uingereza Northampton Town Caleb Chukwuemeka

Jaribio la Aston Villa la kuwasiliana na mshambuliaji wa klabu ya Uingereza Northampton Town Caleb Chukwuemeka limekataliwa. (Mail)

Mlinzi wa North Macedonia Ezgjan Alioski, 29, anatarajiwa kujiunga na Galatasaray kama wakala huru kwa mkataba wa miaka mitatubaada ya kukataa ofa mbili za mkataba mpya kutoka Leeds United. (Football Insider)

Real Madrid wameridhia kuwa mchezaji wa nafasi ya ulinzi Raphael Varane hatasaini mkataba mpya na wanasubiri ofa ya Manchester United. (Goal)

Kiungo wa kati wa Manchester United Jesse Lingard

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Brentford wanajiandaa kuweka mezani ofa ya ya pauni milioni 13.5 kwa ajili ya mlinzi wa Celtic Kristoffer Ajer,23. (Sun)

Mlinzi wa Chelsea Emerson Palmieri,26, anatakiwa na Inter Milan na Roma, huku akiwa chaguo pendwa kwa Napoli wakati pia wakimtolea macho Mathias Olivera, 23, anayekipiga Getafe. (Calciomercato)

Kumsajili mchezaji wa Arsenal Joe Willock,21, kwa mkataba wa kudumu bado imekuwa kipaumbele cha Newcastle United msimu huu baada ya kiungo huyo wa kati, 21, kuwepo St James' Park kwa mkopo msimu uliopita. (Chronicle)

Mlinzi wa Chelsea Emerson Palmieri

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

AC Milan wamekataa zabuni ya pauni milioni 34 kutoka Paris St-Germain kwa ajili ya kiungo wa kati wa Ufaransa Theo Hernandez mwenye miaka 23. (Tuttosport - in Italian)

Inter Milan imeisitiza kuwa kiungo wa kati Nicolo Barella ''hataguswa'' baada ya kuwepo kwa tetesi kuwa mchezaji huyo mwenye miaka 24 ataelekea Liverpool na Manchester United. (Fabrizio Romano on Twitter)

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable