Waholanzi ndio watu warefu zaidi duniani, Je unajua siri ya urefu wao?

 

BBC

Uholanzi ina watu warefu zaidi duniani. Ni ardhi ya watu warefu zaidi duniani: wastani wa urefu wa mwanamume wa Uholanzi ni sentimita 182.5 huku mwanamke akiwa na urefu wa sentimita 168.7. Ukilinganisha na wenzao wa Marekani ambao urefu wao ni semtimita 177.1 na sentimita 163.5 mtawalia.

Lakini sio kwamba hili limekuwa hivi kila siku.

Kwa mujibu wa utafiti katika jeshi la Uholanzi uliochapishwa na shirika maarufu la Royal Society of London ulibaini kwamba katikati ya karne ya 19, wanaume wa Uholanzi walikuwa miongoni mwa watu wafupi zaidi Ulaya.

"Mwaka 1860, urefu wa wanajeshi wa Uholanzi ulikuwa takribani sentimita 165, " Profesa Louise Barrett wa chuo kikuu cha Lethbridge, Canada, ambaye alikuwa sehemu ya utafiti huo, amezungumza na Gavin Haines wa BBC.

"Wakati huo, wanaume wa Marekani walikuwa na urefu wa takriban sentimita 5 zaidi," Barrett aliongeza, na tofauti hii iliwafanya Wamarekani kuwa warefu zaidi duniani.

Hata hivyo, tangu wakati huo kumekuwa na mabadilko makubwa: katika kipindi cha miaka 160 baadaye, wanaume wa Uholanzi wameongeza urefu wao kwa sentimita 20, na kuwapiku wenzao wa Marekani ambao wameongezeka urefu kwa sentimita 6 pekee.

zuecos de distintos tamaños

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Hakuna ushahidi wa kisayansi kuhusu uhusiano wa uubwa wa viatu na urefu wa mtu, ingawa ni ishara ya ukuaji wa mwili ama sehemu ya mwili

"Ukuaji huo ni haraka mno kusema kwamba ni umetokana na chembe za urithi pekee," amesema Barrett, ingawa anaamini kwamba njia ya asili imechangia.

Utafiti wake ulibaini kwamba wanandoa wenye uwezo wa kuzaa sana huko Uholanzi - wale wenye watoto wengi - wana wanaume warefu na wanawake urefu wao ni wa wastani. Na kwa wanandoa wa Marekani hali ikoje? Wanawake ni wafupi na wanaume wana urefu wa wastani.

Sababu za kimazingira pia zimechangia kuongezeka kwa urefu kwa Waholanzi, ameongeza Barrett, akitaja Uholanzi kuwa na mfumo bora wa afya kote duniani, ukosefu wa usawa katika kipato na mfumo bora wa ustawi wa jamii masuala mengine ya wao kuwa na urefu huo kuliko Wamarekani. "[Huko Uholanzi] juhudi zote zilielekezwa katika kuzaa watoto wenye afya ambao hawakuwa na aina yoyote ya matatizo yanayoweza kuchangia kupungua kwa urefu wao," amesema.

Holland

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Urefu au ufupi wa mtoto unachangiwa na aina ya lishe na asili

Jingine linaloweza kuchangia katika kuongezeka kwa urefu ni lishe ya Waholanzi: watu wa Uholanzi wana hamu kweli ya kula vyakula vya maziwa, na utafiti unaonesha kwamba hili limechangia katika kuongezeka kwa urefu wao. "Madini ya Kalisiamu yanaimarisha mifupa na ukuaji unategemea upatikanaji wa madini hayo vizuri mwilini," Barrett amesema.

Kwa mtazamo wetu

Katika utafiti huo, tofauti kati ya nchi ambazo urefu wao ni wa juu na zile ambazo urefu wao ni wa chini ni wastani wa sentimita 20 au zaidi.

Mwandishi mmoja amesema kuwa hili linawakilisha takriban miaka 8 ya pengo la ukuaji kwa wasichana na takriban miaka 6 kwa wavulana.

Hii ina maanisha kuwa wasichana wa Guatemala ambao kwa rekodi ni wafupi zaidi duniani, wakiwa na miaka 19 urefu wao ni sawa na urefu wa wastani wa wasichana wa Uholanzi wakiwa na miaka 11.

Chica en Guatemala

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Wanawake wa Guatemala ndio wafupi zaidi duniani ambao urefu wao ni wastani wa sentimita 150.9

Vilevile, " wavulana wa umri wa miaka 19 kutoka nchi 11 za Asia, Amerika Kusini na eneo la jangwa la Sahara barani Afrika walikuwa na urefu sawa wa wastani kama ilivyokuwa kwa Waholanzi wenye umri wa miaka 13".

Hata hivyo, sote tumekua.

"Kulingana na rekodi zilizopo ni kwamba binadamu wameongezeka urefu katika kipindi cha karne mbili zilizopita," amesema Eirini Marouli, Profesa wa chuo kikuu cha London.

"Na huo ndio ukweli kote duniani.

"Wanaume wamekua kutoka karibu mita 1.60 hadi mita 1.70, wanawake kutoka mita 1.50 hadi karibu mita 1.60," mtaalam wa masuala ya urefu amezungumza na mwanahabari wa BBC Melissa Hogenboom.

"Kwa ujumla tunaweza kusema kuwa wastani wa watu wazima leo hii ni karibu asilimia 5 ya urefu zaidi kuliko jinsi mababu zao walivyokuwa miaka 100 iliyopita."

Hombre demasiado alto para la puerta

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Je wataendelea kuongeza urefu?"Tusubiri tuone ... muda pekee ndio unaoweza kubanisha hilo."

Chembe hizo nyingi za urithi pia zinapatikana ndani au karibu na jeni zinazohusika na ukuaji wa mifupa.

"Baadhi pia wanafafanua zaidi katika mchakato wa kibaolojia unakodhibiti urefu; itafurahisha zaidi kujua namna binadamu anavyokua kuanzia akiwa mtoto hadi mtu mzima huku urefu ukiendelea kuongezeka.

"Na hili limekuwa moja ya maswali magumu zaidi ambalo halijajbiwa kikamilifu.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post