Washukiwa 17 wa mauaji ya rais wa Haiti wakamatwa

0

 


Washukiwa 17 wamekamatwa kufikia sasa kufuatia mauaji ya rais wa Haiti Jovenel Moïse siku ya Jumatano huku mamlaka nchini humo ikisema kuwa washukiwa wawili wanaaminika kuwa na uraia wa nchi mbili za Marekani na Haiti wakati ambapo serikali ya Colombia ikisema kuwa kiasi cha washukiwa sita walihudumu kama maafisa wa jeshi la nchi yake. Mkuu wa idara ya polisi nchini Haiti Leon Charles, amesema jana kuwa washukiwa 15 waliozuiwa ni raia wa Colombia. Charles ameongeza kwamba washukiwa wengine wanane bado wanasakwa na wengine watatu wameuliwa na polisi. Mkuu wa idara ya kitaifa ya polisi nchini Colombia Jenarali Jorge Luis Vargas Valencia, amesema kuwa rais wa nchi hiyo Ivan Duque ameagiza utawala wa jeshi nchini humo pamoja na polisi kushirikiana katika uchunguzi huo. Wakati huohuo, wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema kuwa inafahamu kuhusu ripoti kwamba raia wenye uraia wa Haiti na Marekani wako kizuizini lakini haikuthibitisha wala kusema lolote.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable