Washukiwa watano wafungwa jela Ujerumani kwa kuwadhulumu watoto kingono
Nchini Ujerumani watu wanne wamehukumiwa vifungo vya kati ya miaka 10 na 14 gerezeni baada ya kupatikana na hatia ya kuwalawiti watoto mara kadhaa na kuchukua filamu wakiwafanyia watoto maovu hayo.Mahakama ya mji wa Muenstar magharibi mwa Ujerumani ilitoa hukumu hiyo leo Jumanne ambapo washtakiwa hao pia watakabiliwa hatua za kuwekwa kizuizini baada ya vifungo hivyo.Mama wa mshukiwa mkuu aliyekuwa na umri wa miaka 28, pia alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela baada ya kukutikana na hatia ya kusaidia maovu hayo kufanyika.Kesi hiyo ilichochea mageuzi katika sheria dhidi ya dhuluma za kingono kwa watoto.Jaji katika kesi hiyo Matthias Pheiler alieleza kushangazwa kwake na visa hivyo vya kuvunja moyo na kusema kanda za video zilizoonyeshwa kama Ushahidi zilikuwa za kusikitisha sana.