Watu 45 wauawa katika ghasia za kumuunga mkono Zuma

0

 

45

Watu wapatao 45 wamefariki kwenye ghasia zinazoendelea katika maeneo mbalimbali nchini Afrika Kusini, tangu kujisalimisha kwa rais wa zamani wa nchi hiyo, Jacob Zuma wiki iliyopita.

Karibu watu 800 wamekamatwa katika ghasia hizo zilizoanza kama maandamano alhamisi iliyopita kupinga kwenda jela kwa Zuma.

Lakini waandamanaji waligeuza maandamano hayo na kuwa ghasia mwishoni mwa wiki, wakichoma moto, kufunga barabara kuu na kuvamia na kupora maduka.

south

Jeshi limepelekwa katika maeneo mbalimbali kuongeza nguvu na kusaidiana na Polisi kuzima ghasia hizo.

Waziri wa Polisi Bheki Cele amewaambia waandishi wa habari jana leo kwamba uporaji unaendelea na ipo hofu kwamba, kuna baadhi ya maeneo yatakuwa na uhaba wa bidhaa za msingi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable