Abba Kyari anasifika sana nchini Nigeria kwa kuwa "polisi mchapa kazi".
Ni afisa wa polisi aliyetunukiwa tuzo nyingi zaidi kwa kuchunguza kesi kubwa za uhalifu. Na hujumuika sana na wanasiasa na watu mashuhuri.
Mienendo ya Bw. Kyari sasa inachunguzwa tangu vyombo vya sheria vya Marekani kuonyesha kwamba anatafutwa kuhusiana na madai ya kuhusishwa na mshawishi na tapeli wa Instagram Ray Hushpuppi.
Afisa huyo wa polisi amekanusha kufanya hatia yoyote.
Wakosoaji wa Bw. Kyari, hawajatilia shaka madai hayo. Wanasema afiso mwenye miaka 46 - aliyetambuliwa na Rais Muhammadu Buhari kama shujaa - aliwahi kukabiliwa na madai ya ufisadi na ukiukaji wa haki za binadamu nchini Nigeria.
Bw Kyari, ambaye anashikilia cheo cha naibu kamishena wa polisi amepuuzilia mbali madai hayo akisema ni ya uwongo na kwamba hakuna hatua yoyote ishawahi kuchukuliwa dhidi yake kuhusiana na madai hayo.
Kusimamishwa na polisi
Ken Henshaw, mkuu wa shirika la kutetea haki la We The People, amesema Bw. Kyari had been rewarded by a system based on patronage which, in some cases, even punished people with integrity.
"Madai dhidi yake yanalingana na yale ambayo yametolewa dhidi ya polisi wa Nigeria, na maafisa wake wa ngazi za juu siku zilizopita, "alisema Bw Henshaw.
Lakini Kamishena wa polisi wa Nigeria amelazimika kumsimamisha kazi Bw. Kyari.
hatua ambayo inajiri baada ya Marekani wiki iliyopita kutangaza kwambai meanzisha mashtaka dhidi yake kufuatia madai kuwa aliwezesha malipo kwa wafanyikazi wa polisi wa Nigeria kutoka Hushpuppi, ambaye jina lake halisi ni Ramon Abbas.
BBC imewasiliana na Bw. Kyari kupata tamko lake.
Ray Hushpuppi - au Hush kama anavyofahamika na wafuasi wake - alionesha maisha yake ya kifahari kwenye mtandao w Instagram
Hushpuppi - ambaye alikuwa na mashabikii milioni 2.4 kwenye Instagram - alikiri mashtaka ya utapeli wa pesa huko Marekani baada ya kusafirishwa kutoka Dubai mwaka jana.
Akijinadi kama mwanabiashara katika jimbo la Ghuba Mnageria huyo mwenye umri wa miaka 37-mara nyinge aliweka mtandaoni picha za maisha yake ya kifahari na alikuwa na kitengo cha video alichokiita Flexing - lugha ya mtandao wa kijamii inayoashiria kujionesha.
Lakini alikuwa sehemu ya wahalifu wa kimtandao ambao waliwatapeli watu na mashirika karibu dola milioni 24, nyaraka za mahakama zilidai.
'Pesa za Hushpuppi zilikuwa za nguo'
Maafisa wa Marekani wanadai katika hati ya kiapo kwamba Hushpuppi alimfanya Bw Kyari amkamate Vincent Chibuzor, ambaye alikuwa wametofautiana naye.
Bw. Kyarianadaiwa kumtumia Hushpuppi maelezo ya akauti ya benki kulipia kukamatwa huko,taarifa ilisema.
Katika majijibu ambayo yamefutwa katika ukurasa wa Facebook yalielezea kuwa madai hayo ni ya "uwongo" na kusema kwamba Hushpuppi alikuwa analipia nguo aliyokuwa ameshonewa.
- "Aliona nguo za kinyumbani na kofia katika ukurasa wa mtandao wa kijamii na kuzipenda," alisema katika ujumbe wa Facebook, akiongeza kuwa Hushpuppi alituma pesa za kushonewa nguo.
Hati ya mahakama ya Marekani iliyowasilishwa na FBI inaonyesha maelezo ya madai ya mazungumzo ya WhatsApp kati ya polisi na yule mtu maarufu wa utapeli wa Instagram.
Ujumbe huo unadai kwamba Hushpuppi alilipa naira milioni 8 sawa na (dola 19,000; Pauni 14,000) kwenye akaunti zilizobainishwa na polisi wa Nigeria ambayo maelezo yao yalitolewa na Bw Kyari, kumzuilia Bw Chibuzor.
'Hakuna mtu aliyedai pesa'
Katika ujumbe mmoja, Hushpuppi anadaiwa kusema: "Mkuu nifahamishi jinsi nitakavyowasilisha pesa kwa timu yako. Nataka wamchukulie hatua kama mwizi aliyejihami," ambapo Bw. Kyari aliripotiwa kujbu: "SAWA nitakutumia maelezo yao."
Bw. Kyari pia amekanusha kufuta ujumbealiyoweka Faceboo.
"Hakuna mtu aliyedai pesa yoyote kutoka kwa ... Hushpuppi na hakuna mtu aliyepokea pesa yoyote kutoka kwake."
Badala yake alisema, alikuwa akijibu ombi la dharura kutoka kwa Hushpuppi ambaye alidai kulikuwa na tishio lililolewadhidi ya familia yake.

