Hiroshima yaadhimisha kumbukumbu ya miaka 76 ya bomu la nyuklia

0

 


Mji wa Hiroshima leo Ijumaa unaadhimisha kumbukumbu ya miaka 76 tangu uliposhambuliwa na bomu la nyuklia. Meya wa mji huo amewahimiza viongozi duniani kuungana kuondoa kabisa silaha za nyuklia kama walivyoungana sasa hivi katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona.


Meya Kazumi Matsui amewatolea wito viongozi duniani kujitolea kuondoa silaha za nyuklia kama jinsi wanavyokabiliana na janga la ugonjwa wa Covid-19 ambao jamii ya kimataifa unauona ugonjwa huo kama tishio kwa binadamu."Naihimiza serikali ya Japan kutia saini mkataba wa kuzuia silaha za nyuklia na kushiriki katika mkutano wa kwanza wa nchi zenye silaha za nyuklia. 


Japan inapaswa kuwa mpatanishi kati ya nchi zenye silaha za nyuklia na zisizokuwa na silaha hizo kwa kuweka mazingira ya kuamianiana na usalama bila ya kutegemea silaha za nyuklia."Marekani iliishambulia Hiroshima kwa kurusha bomu la kwanza la atomiki duniani mnamo Agosti 6, mwaka 1945 na kufanya uharibifu katika mji huo na kuua watu 140,000.


Marekani ilirusha bomu la pili siku tatu baadaye katika mji wa Nagasaki lililowaua watu wengine 70,000. Japan ilisalimu amri Agosti 15, na kumaliza vita vikuu vya pili vya dunia.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable